Afisa Elimu na Huduma kwa walipa kodi TRA mkoa wa Shinyanga, Semeni Mbeshi akitoa elimu ya kodi,Matumizi ya mashine za kielektroniki za kutolea risiti (EFD Mashine) na mfumo wa kodi ya ongozeko la thamani (VAT) kwa wachimbaji na wafanyabiashara wakata ya mwaktolyo halmashauri ya Shinyanga.

****
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeendesha semina ya Elimu ya Kodi,matumizi ya mashine za EFD na mfumo wa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwa Wachimbaji wamadini waliopo katika kata ya Mwaktolyo namba 5 halmashauri ya wilaya ya Shinyanga mkoani humo kwalengo la kuwajengea uelewa wafanyabiashara na wachimbaji juu ya umuhimu wa kulipa kodi kwa hiari.
Semina hiyo ya siku moja imefanyika Jumanne 13,2022 katika eneo la stendi kata ya Mwakitolyo na kuhudhuriwa na wachimbaji wamadini pamoja na wafanya biashara mbalimbali wakiwemo wafanyabishara wa madini.
Afisa Elimu na Huduma kwa walipa kodi TRA mkoa wa Shinyanga, Semeni Mbeshi amesema lengo la semina hiyo ni kuwajengea uelewa wachimbaji na wafanyabisahara kuhusu masuala a Kodi,Matumizi ya mashine za kielektroniki za kutolea risiti (EFD Mashine) na mfumo wa kodi ya ongozeko la thamani (VAT).
"Tumekutana na wachimbaji pamoja na wafanyabiashara kwani tunaamini kuwa wachimbaji na wafanyabiashara ni wadau muhimu wakielewa vizuri kuhusu masuala ya kodi watasaidia pia kuielimisha jamii inayowazunguka ",amesema Semeni
Social Plugin