Polisi nchini Msumbuji imewakamata vijana 29 wanaosadikiwa kusafiri ili kujiunga na vikosi vya kijihadi katika jimbo lenye utajiri wa gesi la Cabo Delgado.
Vijana hao ambao wengi ni wadogo kiumri wakitokea katika wilaya za Memba na Nacala-Porto karibu na jimbo la Nampula , wamesema kwamba walikua wakielekea Cabo Delgado kwa ajili ya shuguli za uvuvi.
Msemaji wa polisi wa Nampula , Zacarias Nacute amesema kwamba vijana hao waliahidiwa ajira na makundi hayo ya kijihad.
Wanatarajiwa kuchukuliwa hatua za kisheria ambapo wameshakabidhiwa kwa mwendesha mashatka mkuu wa serikali. Msumbuji imekua kwenye mapambano dhii ya vikosi vya kijihadi tangu mwaka 2017.
Social Plugin