Mwanamume aliyewalaghai makumi ya wanawake kumtumia picha za sehemu zao za siri akijifanya daktari wa wanawake kwenye Facebook, amefungwa jela nchini Singapore.
Mahakama Kuu siku ya Jumatano Oktoba 26,2022 ilimpata Ooi Chuen Wei, 37, kutoka Malaysia, na hatia ya kujifanya mtu mwingine kumhukumu kifungo cha miaka mitatu na miezi minne jela.
Kulingana na hati za mahakama, Ooi anaripotiwa kutumia akaunti feki kwenye Facebook kuwasiliana na wanawake hao, akiwataka kujaza tafiti zilizojumuisha maswali kuhusu sehemu zao za siri na maisha yao ya kingono.
Kwa kipindi cha miaka minne, aliwahadaa wanawake 38 na kupokea karibu picha na video 1,000 za ngono kama malipo.
Siku ya arobaini
Siku za arobaini za Wei zilifika mnamo Julai mwaka jana wakati mwanamke mmoja ambaye alikuwa anamshuku kugundua kuwa hakuna daktari mwenye jina kama hilo na kupiga ripoti kwa polisi.
Kisha polisi walivamia nyumba ya Ooi na kukamata vifaa vyake vya kutekeleza njama yake chafu.
Wakati wa uchunguzi wa polisi, alikiri kwamba aliwahadaa wanawake hao, CNN inaripoti.
Alikabidhiwa kifungo hicho baada ya naibu mwendesha mashtaka wa umma R. Arvindren kuomba korti imfunge jela kwa angalau miaka mitatu na miezi minane akitaja idadi kubwa ya waathiriwa na muda ambao Ooi alikuwa ameendeleza udanganyifu wake.
Arvindren alisema mshtakiwa alitekeleza mpango uliobuniwa kwa makini ili kunufaisha tamaa zake za ngono.
"(Yeye) alijifanya kuwa daktari wa kike na kuwahadaa waathiriwa kadhaa kutuma picha na video zao chafu.
(Yeye) ametumia vibaya imani ya umma kwa madaktari na ametumia mitandao ya kijamii kutekeleza uhalifu huo,” aliongeza.
Social Plugin