Zaidi ya dozi 20,000 za chanjo ya majaribio dhidi ya ugonjwa wa Ebola aina ya Sudan ambao umeikumba nchi ya Uganda zinatengenezwa nchini india.
Taarifa zinasema kwamba chanjo hizo zinaweza kutengenezwa na Taasisi ya Serum ya India na kutumika katika majaribio kuona kama zinaweza kufanya kazi ya kukabiliana na mlipuko wa sasa nchini Uganda.
Chanjo kadhaa zimetumwa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo dhidi ya aina ya hiyo ya Ebola, lakini hakuna chanjo iliyothibitishwa yenye ufanisi dhidi ya aina ya Sudan.
Watu 19 wamefariki kufikia sasa na kumekuwa na visa 54 vilivyorekodiwa tangu kuzuka kwa janga hilo mwezi uliopita.
Mwishoni mwa wiki, Rais Yoweri Museveni aliweka aliziweka karantini wilaya mbili
Social Plugin