Mkuu wa kitengo cha Jiolojia kutoka Geita Gold Mining Limited (GGML), Eric Kalondwa (kulia) akipokea tuzo ya mdhamini bora wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Watalaam wa Jiolojia (GST) kutoka kwa
Waziri wa Madini, Dk. Doto Biteko (kushoto). Kalondwa alipokea tuzo hiyo kwa niaba ya GGML kampuni ambayo imekuwa ikidhamini mkutank huo kila mwaka. Mwaka huu umefanyika jiji Arusha.
Katika kuunga mkono ukuaji wa fani mbalimbalinchini, Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imejitosa kudhamini mkutano mkuu wamwaka wa wanajiolojia wa Tanzania unaofanyika mkoani Arusha.
Mkutano huo ambao umeanza tarehe 4 Oktobaunatarajiwa kumalizika tarehe 7 Oktoba mwakahuu na unaratibiwa na Chama cha Watalaamwa Jiolojia Tanzania (TGS) kinachokadiriwakuwa na wanachama zaidi ya 300.
Akizungumza na Mwandishi wetu, Mrakibu waJiolojia katika Kampuni ya GGML, Eric Kalondwa alisema kampuni ya GGML imetoashilingi milioni 25 za Kitanzania kudhaminimkutano huo uliofunguliwa na Waziri waMadini, Dk. Dotto Biteko kwa niaba ya Makamuwa Rais, Dkt. Philip Mpango lakini unatarajiwakufungwa na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso.
Alisema katika mkutano huo ambao hufanyikakila mwaka kwenye mikoa tofauti tofauti, jumlaya wanajiolojia 11 kutoka mkoani Geita wameshiriki.
Aliongeza kuwa mkutano huo umelengakubadilishana uzoefu kwa sababu kunaprogamu mbalimbali zinazolenga kuwawekapamoja watu wenye fani zinazofanana.
Alisema wafanyakazi wa GGML ambao pia niwana fani hiyo ya jiolojia, wamefaidika kwanamna mbalimbali tangu kianzishwe chama hicho.
Alisema mkutano wa mwaka huu unalengakukazia suala la upatikanaji wa bodi yawanajiolojia hasa ikizingatiwa fani hiyoinajumuisha watu kutoka maeneo mbalimbaliikiwamo wanaofanya kazi kwenye uchimbaji wamafuta, kwenye maji, madini ya aina mbalimbalitofauti na na dhahabu.
Hata hivyo, alikiri kuwepo kwa changamoto yauhaba wa wanawake kusomea fani hiyo, lakiniakawatia shime wanawake kusomea fani yajiolojia kwani haihitaji kuwa na nguvu kubwa ilikukidhi vigezo vya kuwa mwanajiolojia.
“GGML kwa kweli inafanya vizuri sanakuendeleza ma-jiolojia toka wanapokujakujifunza kwa vitendo na wanaokuja kazini. Wale wanaopitia kwenye mgodi wetu hakikawanawasifia kwa mapokeo makubwatunayowapatia kulingana na program ya mwakaambayo huwa tunawaandalia,” alisema.
Wanajiosayansi ni wataalam waliosomea nawenye uzoefu wa fani za jiolojia (miamba), jiofizikia, jiokemia, jioteknolojia na jiolojia yamazingira na nyinginezo.
Awali akifungua mkutano huo, Waziri wa madini Dk. Biteko alisema wizara iko katika hatua za mwisho za kukamilisha mchakato wakuanzishwa kwa bodi ya wanajiolojia nakuongeza kwamba, baada ya Serikalikukamilisha sehemu yake,itatoa nafasi kwa wadau kutoa maoni kuhusu namna gani bodihiyo iundwe, namna itakavyosimamiwa, masuala yatakayohusisha vyanzo vya fedha nakuangalia masuala ya sheria.
Aliongeza kuwa, wakati Serikali inakamalimishamchakato wa kuundwa kwa bodi ya wanajiolojia ni muhimu wajiolojia wakahakikisha wanaiendeleza taaluma yajiolojia ili kuipatia nchi heshima ikiwemo kuwawezesha wawezekaji kupata taarifa sahihina hivyo kuvutia uwekezaji zaidi kwenye sektaya Madini.
Pia aliwataka Wajiolojia nchini kuhakikisha wanaiheshimisha taaluma yao kwa kutoruhusu wasio waaminifu kuingilia majukumu yakitaaluma kutokana na umuhimu wa shughuliza utafiti kwa maendeleo ya Sekta ya Madini naTaifa.
Aidha, Rais wa Chama cha Wataalam wajilojiaTanzania, Prof. Abdulkarim Mruma aliieleza hadhira kuhusu utajiri wa kijiolojia ambao nchiya Tanzania imebarikiwa kuwa nao na kuelelezea namna bora ya kuitumia taalumahiyo kwa maendeleo ya nchi na jamii nzima.