Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugeni wa Kampuni ya Gewoma Goldmine Company Limited Bi. Josepha Woiso (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wengine wa Kampuni hiyo wakiwa kwenye Banda lao katika Maonesho ya Teknolojia katika Sekta ya Madini Mkoani Geita. (wa kwanza kulia) ni, Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo Hellen Maduhu. wengine ni wajumbe wa Bodi wa Kampuni hiyo. (Kutoka kushoto), ni Johnson Manyanga, (anayefuata) ni, Honoratha Shirima, Kang’wa Mushosha, na Afisa Masoko wa Kampuni hiyo Geremia Ndaki.
Gewoma Goldmine Company Limited ni kampuni ya wachimba madini mkoani Geita ambayo hivi Sasa imewekeza kwenye uchimbaji wa madini ya viwanda aina ya Kaolin.
Madini ya Kaolin yanatumika kutengeneza bidhaa mbalimbali za viwandani ikiwemo saruji, vyombo vya udongo, vigae, rangi za nyumba, dawa, mbolea dawa za mswaki.
Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni hiyo Hellen Maduhu amesema anayo furaha kushiriki katika maonyesho ya tano ya teknolojia ya madini na kuwa Kampuni pekee iliyoweza kuonyesha madini aina ya Kaolin yanayotumika katika uzalishaji wa bidhaa za viwandani.
Kutokana na uwepo wa utajiri mwingi wa madini aina ya Kaolin Kanda ya ziwa ambayo kampuni hiyo imeyabaini, Kampuni Sasa inakaribisha wawekezaji mbalimbali wa viwanda vya saruji, vigae na malighafi nyinginezo ili kuwekeza