Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA amewataka viongozi wa chama hicho kuendelea na mandalizi ya mikutano ya hadhara nchi nzima huku akisema chama hicho kitatangaza tarehe rasmi ya kuanza mikutano ya hadhara.
Kauli ya John Mnyika ameitoa jana wakati akizungumzia ripoti ya kikosi kazi kilichoundwa na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambapo moja kati ya mambo yaliyoibuliwa ni suala la mikutano ya kisiasa ya hadhara
"Mikutano ya hadhara zuio haramu liondolewe, kwa kauli ya Rais bila kusubiri marekebisho ya kanuni na sheria, na wakati kauli hiyo ikisubiriwa ngazi zote za chama ziendelee na maandalizi ya mikutano ya hadhara"
Rais wa Tanzania akipokea ripoti hiyo ya kikosi kazi jana Aktoba 21 alisema suala la mikutano ya hadhara linahitaji kutupiwa jicho kanuni zake za mwaka 2019 ili kuondoa madhara yanayoweza kujitokeza.
Via EATV