Mgeni Rasmi Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile ( wa pili kulia),Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Little Treasures, Paul Ikelege na wahitimu wa elimu ya darasa la saba wakikata keki maalumu wakati wa Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga yamefanyika leo Jumamosi Oktoba 15,2022 ambapo jumla ya wanafunzi 105 kati yao wavulana 54 na wasichana 51 wamehitimu elimu ya msingi mwaka 2022.
Akizungumza wakati wa mahafali hayo, Mgeni Rasmi Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Sophia Mjema ameipongeza shule ya Msingi Little Treasures kwa maendeleo mazuri katika elimu na kuupa heshima mkoa huo.
“Serikali inathamini sana sekta binafsi katika utoaji wa elimu bora ndiyo maana imekuwa ikitoa miongozo mbalimbali ya namna ya kusimamia elimu katika sekta binafsi. Shule binafsi zinasaidiana na elimu. Serikali ya mkoa wa Shinyanga inaendelea kushirikiana na wadau wa elimu ili kuboresha elimu nchini”, amesema Dkt. Ndungile.
“Tunalo jukumu la kuwajengea vijana maadili na malezi bora. Suala la malezi, utamaduni na mila katika shule zetu lazima vipewe kipaumbele katika shule zetu na tuendelee kufundisha somo la dini shuleni ili watoto wetu wawe na hofu ya Mungu na wamche Mungu”,amesema Dkt. Ndungile.
Amesema serikali imeendelea kutoa fedha nyingi kwa ajili ya kuboresha miundo mbinu ya shule huku akisema upo umuhimu mkubwa kufundisha somo la TEHAMA katika shule.
“Dunia inabadilika, mambo yanabadilika, naomba somo la TEHAMA tulipe kipaumbele. Ulimwengu wa sasa ni ulimwengu wa sayansi na teknolojia hivyo ni lazima waelewe masuala ya teknolojia. Lakini tuwapatie elimu ya ujasirimali ambayo itawaidia kadri wanavyokua”,ameongeza Dkt. Ndungile.
Amewashukuru wazazi kwa kuweka misingi mizuri ya elimu kwa wanafunzi huku akiwataka kutimiza wajibu wao kwa kulipa ada kwa wakati.
Wahitimu wakitoa burudani kwenye Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures 2022.
Mkurugenzi wa Shule za Msingi na Sekondari Little Treasures, Lucy Mwita amesema tangu shule ya Msingi Little Treasures ilipoanzishwa mwaka 2012 imeendelea kufanya vizuri kwenye mitihani ya taifa na imekuwa ikipata wanafunzi katika uwiano sawa kati ya wasichana na wavulana na matokeo yanatoka sawa ukiwa mzuri kwa kufaulisha wanafunzi wote kwa kupata daraja A tangu mwaka 2017 hadi mwaka 2021.
“Hapa Little Treasures pia tuna Shule ya Sekondari Little Treasures, tunawakaribisha sana wanafunzi wanaotarajia kuanza masomo ya Kidato cha kwanza mwaka 2023. Hawa wanafunzi waliomaliza elimu ya darasa la saba hapa naomba wazazi muwalete wanafunzi hawa tuendelee nao lakini pia tunazo nafasi za masomo kwa elimu ya awali, waleteni hapa ili wapate elimu bora kwani shule yetu ni Bora na kuna mazingira rafiki ya kujifunzia na kufundishia. Tumewalea kwa upendo mkubwa na tumewafundisha mambo mazuri ya kijamii na kitaaluma”,amesema Lucy.
“Pia tumeanzisha Kituo cha afya hapa shuleni kwa ajili ya kuhudumia wanafunzi wetu pindi wanapopatwa na changamoto za kiafya ambapo tunaye Daktari Bingwa wa watoto”,ameeleza Mkurugenzi wa shule za Little Treasures.
Meneja wa shule za Little Treasures Alfred Mwita amesema shule za Msingi na Sekondari Little Treasures zimekuwa chachu kubwa katika sekta ya elimu mkoa wa Shinyanga na taifa kwa ujumla huku akiahidi kuwa wataendelea kuboresha zaidi shule na elimu.
“Huu ni mwaka wa 11 tangu tulipoanzisha shule ya msingi Little Treasures tukiwa na wanafunzi wanne tu na sasa tuna jumla ya wanafunzi 776 wa darasa la kwanza hadi la saba. Kutokana na kukubalika kwa Little Treasures ndiyo maana idadi ya wanafunzi imekuwa ikiongezeka kila mwaka. Tumejipanga ndani ya miaka 10 ijayo tutakuwa na mabadiliko makubwa kuliko miaka 10 iliyopita. Dhamira yetu ni kuwa shule bora inayotoa elimu bora”,amesema Mwita.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mgeni Rasmi Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akizungumza wakati wa Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mgeni Rasmi Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akizungumza wakati wa Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa Shule za Msingi na Sekondari Little Treasures, Lucy Mwita akisoma taarifa ya shule ya Msingi Little Treasures wakati wa Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.

Meneja wa shule za Little Treasures Alfred Mwita akizungumza wakati wa Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Meneja wa shule za Little Treasures Alfred Mwita akizungumza wakati wa Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Mgeni Rasmi Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile (kulia) ,Mkurugenzi wa Shule za Msingi na Sekondari Little Treasures, Lucy Mwita (katikati) na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Little Treasures, Paul Ikelege (kushoto) wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures.
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Little Treasures, Elizabeth Mokoni akisoma risala ya shule wakati wa Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Little Treasures, Paul Ikelege.
Wahitimu wakiwa kwenye Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures 2022.
Mgeni Rasmi Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile ( wa pili kulia), Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Little Treasures, Paul Ikelege na wahitimu wa elimu ya darasa la saba wakikata keki maalumu wakati wa Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Mgeni Rasmi Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile ( wa pili kulia),Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Little Treasures, Paul Ikelege na wahitimu wa elimu ya darasa la saba wakikata keki maalumu wakati wa Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Mgeni Rasmi Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile (kulia) akimlisha keki mmoja wa wahitimu wa elimu ya darasa la saba wakati wa Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.

Mgeni Rasmi Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile (kulia) akimlisha keki Mkurugenzi wa Shule za Msingi na Sekondari Little Treasures, Lucy Mwita wakati wa Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Mgeni Rasmi Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile (kulia) akimlisha keki Meneja wa shule za Little Treasures Alfred Mwita wakati wa Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Little Treasures, Paul Ikelege akimlisha keki Mgeni Rasmi Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile (kulia) wakati wa Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Mgeni Rasmi Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile akigawa vyeti kwa wahitimu wa elimu ya darasa la saba wakati wa Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.

Meneja wa shule za Little Treasures Alfred Mwita akicheza muziki wakati wa Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Wazazi na wageni waalikwa wakiwa kwenye Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures
Wahitimu wakiwa kwenye Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures 2022.
Wahitimu wakitoa burudani kwenye Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures 2022.
Wahitimu wakitoa burudani kwenye Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures 2022.
Wanafunzi wakitoa burudani kwenye Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures 2022.
Walimu wakicheza muziki kwenye Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures 2022.
Wanafunzi wa Kidato cha nne shule ya Sekondari Little Treasures wakiimba wimbo maalum kwenye Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures 2022. Kushoto ni Meneja wa shule za Little Treasures Alfred Mwita, kulia ni Mkurugenzi wa Shule za Msingi na Sekondari Little Treasures, Lucy Mwita.
Meneja wa shule za Little Treasures Alfred Mwita (kulia) ,Mkurugenzi wa Shule za Msingi na Sekondari Little Treasures, Lucy Mwita (kushoto) na walimu wa shule ya msingi Little Treasures wakicheza muziki.
Wazazi na wageni waalikwa wakiwa kwenye Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures
Wanafunzi wakiimba wimbo maalumu kuhusu mama wakati wa Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures
Wanafunzi wakitoa burudani wakati wa Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures
Wazazi na wageni waalikwa wakiwa kwenye Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures
Wanafunzi wakitoa burudani wakati wa Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures
Wanafunzi wakitoa burudani wakati wa Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures
Mwakilishi wa wazazi, Herieth Nkya (kulia) akizungumza mbele ya walimu waliofundisha wanafunzi wa darasa la saba mwaka 2022 wakati wa Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Wazazi na wageni waalikwa wakiwa kwenye Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures
Wanafunzi kidato cha nne shule ya Sekondari Little Treasures wakitoa burudani wakati wa Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures
Wazazi na wageni waalikwa wakiwa kwenye Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures
Wazazi na wageni waalikwa wakiwa kwenye Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures
Wazazi na wageni waalikwa wakiwa kwenye Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures
Wazazi na wageni waalikwa wakiwa kwenye Mahafali ya sita ya Darasa la Saba Shule ya Msingi Little Treasures
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog