Kisura mmoja kutoka Nigeria, @aphrodite_zee, kwenye TikTok, ameshiriki masaibu yake ya kuhuzunisha na mashabiki huku akiwaomba ushauri wa jinsi ya kushughulikia hali yake.
Mwanamke huyo alisimulia jinsi alivyoolewa na mume wake mpendwa miaka mitatu iliyopita, na mambo yalikuwa yakienda sawa wakati huo.
Muda mfupi baadaye kwa masikitiko, mume wake alianza kuwa na ujeuri na kumpiga mara kadhaa.
Alipata mimba yake na mambo yakawa mabaya zaidi. Alianza kuhusiana kimapenzi na mwanamke mwingine na kumtelekeza.
Mrembo huyo kwa majonzi alirejea nyumbani kwa wazazi wake ambapo alijifungua. Kwa takriban miaka miwili, hakuwajali na wala hata kuwatembelea.
Aphrodite_zee, hata hivyo alifichua kuwa jamaa sasa amechukua abautani kwani anataka warudiane.
Alisema amekuwa akifanya juhudi za kurudiana naye na mtoto ili wawe familia tena.
"Miaka mitatu iliyopita nilikuwa nimeolewa. Kila kitu kilikuwa kikienda vizuri hadi alipoanza kunipiga. Nilipata mimba hatimaye.
Alinipuuza na kuanza mahusiano na mwanamke mwingine. Nilirudi nyumbani kwa mzazi wangu na kujifungua mtoto wangu. Sasa hivi tumeishi miaka miwili bila yeye kutujulia hali. Nimesonga mbele lakini sasa anataka turudiane na kumlea mtoto wetu," ujumbe wake ulisema.
Haya ni ni baadhi ya maoni ya watu mitandaoni;
@user3816330497881 alisema: "Mwanaume anapompiga mwanamke mara moja, hawezi kuacha, endelea na maisha yako kwa vile hakuwepo hapo awali, Mungu yu pamoja nawe."
@777_222_5 aliandika: "Hakuna kitu cha kukufanya uchanganyikiwe hapo. Shirikianeni kumlea mtoto wenu ila usirudi nyuma katika maisha yake tena. Wewe ni mrembo na utapata mtu."
@precious__gold123 alisema: "Dadangu nilifanya vivyo hivyo aliporudi na nilimsamehe lakini sikuwa na furaha wala amani. Hata nilipoteza mtoto wangu wa pili kwa sababu yake na sasa ninaishi maisha yangu kivyangu."
@ruhashaz alisema: "Usifanye hivyo mpenzi! Wewe ni mwanamke mrembo na jasiri. Usiruhusu aingie tena katika maisha yako. Atakuangamiza tena na safari hii wewe na mwanao mtashikwa na kiwewe."
Social Plugin