Inawezekekana kuwa ni kitu cha kustaajabisha, lakini ndio ukweli wa mambo kwa Garry Richmond, mwanaume aliyepoteza fahamu na baadae kuvutiwa na kumuoa aliyekuwa mke wake kwa mara ya pili bila ya kujua.
Inaelezwa kuwa Garry Richmond, alipoteza fahamu kwa muda mrefu na baada ya kuzinduka hakuwa na kumbukumbu yoyote, na hayo yote yalitokea baada ya kupigwa na vijana wakati akituliza vurugu walizokuwa wakizifanya walipokuwa wakitazama mpira kwa pamoja, na ilikuwa ni kilele cha kombe la Dunia.
Baada ya tukio hilo ilimpelekea matatizo kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata kichwani na kuvunjwa bega, hospital kuligeuka nyumba yake mpya, na ‘oksijeni’ ilikuwa ndio masada wake katika kupata pumzi.
Baada ya mda mrefu kuwa hospitalini, siku aliyopata fahamu hakuweza kumfahamu kabisa mkewe wala mtoto wake, licha ya kuishi na mkewe huyo kwa miaka 20 ya Ndoa.
Kutokana na huduma alizokuwa akipatiwa na Karen aliyekuwa Mke wake, na ukarimu aliomuonesha kipindi chote alipokuwa Hospitalini, Garry alijikuta akivutiwa na mwanamke huyo na kumtongoza tena bila kufahamu kuwa alikuwa mkewe wa halali, na haikuwa ngumu kwa Karen .
Baada ya miaka mitatu Garry, afya yake iliimarika sawa sawa alimuoa tena Karen kwa ndoa ya pili.
Social Plugin