Video iliyomnasa Pasta James Ng'ang'a akiyaondoa mapepo kutoka kwa waumini wake, imewasha mitandao ya kijamii huku wengi wakishangaa iwapo ni kweli au walikuwa wakiigiza.
Kwenye video fupi iliyosambazwa na katika Facebook na Channel 7 News, wanawake walianza kuanguka kwenye madhabahu baada ya Ng'ang'a kukemea kwa jina la Yesu Kristo.
Mtandao huu haujabainisha ni nini kilichokuwa kikiendelea ila kwa kukagua video hiyo, pasta huyo alionekana kuoyaondoa mapepo.
Waumini hao, wengi wakiwa ni wanawake walianza kufoka na kupagawa kwenye madhabahu, huku Ng'ang'a akiwashabikia.
Baadhi ya wanaume walijiunga kwenye sarakasi hizo na kuanza kupiga miereka, na kuzidi kufanya wengi kuchanganyikiwa hata ingawa hawakuumizana.
Matukio hayo yalionekana ni kama mchezo wa kuigiza, na dakika za mwisho Ng'ang'a aliwaambia walisifu jina la Yesu Kristo.
Wakenya watoa maoni kuhusu video hiyo.
Mohamed Hussein Saadad: "Nijuavyo, ukiamini umepona basi umepona tayari. Haihusiana kivyovyote na miujiza au pasta Nganga."
Mboya Denis: "Sasa vitimbi vya nini? Ninachoona na mchezo wa kuigiza huku kukiwa na waigizaji waliopewa mafunzo. Hongera pasta nganga."
Edson Bukenya: "Afrika imejaa vitimbi, ni Mungu aingilie kati!"
James Lukindo: "Hiyo ni drama ya miujiza kwenye makanisa pekee. Ikiwa ni kweli wanaponya na kukemea mapepo kwa nini wasiendee hospitalini ambako watu wengi wanateseka?"
Social Plugin