Wananchi wakishiriki mazishi ya Nshoma Moshi
**
Watu wawili wakazi wa Kata ya Didia, Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, wamefariki dunia akiwemo mama mmoja aitwaye Nshoma Moshi, aliyekatwa mapanga akiwa nyumbani kwake majira ya saa 2:00 usiku wakati akimuogesha mjukuu wake.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi, amesema kwamba tukio hilo limetokea Oktoba 29, 2022, na uchunguzi wa awali umebaini kwamba mwanamke huyo aliuawa kutokana na changamoto za migogoro ya ardhi.
Kufuatia tukio hilo Kamanda Magomi, ameonya tabia ya watu kujichukulia sheria mkononi likiwemo tukio la kijana Willson Jogoo(30), aliyeuawa na wananchi wenye hasira kali, katika Kijiji cha Chembeli baada ya kuiba kuku.
CHANZO - EATV
Social Plugin