Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAJAMBAZI WAVAMIA KANISA, WAPORA MALI NA KUMUUA PASTA


Kundi la Wakristu waliokuwa wamekusanyika kusali katika eneo la Diepsloot, Afrika Kusini waligeuka kuwa waathiriwa wa wizi wa kimabavu baada ya majambazi kuwavamia na kumuua pasta wao.


Kulingana na ripoti, waumini wawili walijeruhiwa vibaya wakati wa kisa hicho cha kutamausha.

 News24 inaripoti kuwa kisa hicho kilitokea muda mfupi kabla ya saa usiku. 

Ripoti zinaonyesha kuwa Wakristu 50 walikuwa wamekusanyika katika kanisa lao kwa ajili ya maombi na kukesha wakati majambazi hao wenye silaha walipowashambulia.

Inasemekana kuwa majangili hao walitoroka na mali zao za thamani kama vile simu na pesa taslimu.

 Watu watatu akiwemo pasta walipigwa risasi wakati wa shambulio hilo na kukimbizwa kwenye kituo cha afya cha karibu, lakini pasta alifariki dunia alipofika hospitalini. 

Waathiriwa wengine wawili wanasemekana kuwa katika hali sawa. 

Msemaji wa polisi wa Diepsloot, Luteni Kanali Mavela Masondo alithibitisha tukio hilo na kueleza kuwa msako wa kuwasaka wahalifu hao umeanzishwa. 

Vile vile aliongeza kuwa kesi za mauaji na jaribio la kuua zimefunguliwa. "Watu watatu waliopigwa risasi, akiwemo mchungaji, walipelekwa katika kituo cha matibabu cha eneo hilo ambapo pasta alifariki alipofika. Wengine wawili wako katika hali mbaya lakini inaendelea vizuri."

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com