Aliyekuwa mgombea wa ujumbe wa mkutano mkuu Taifa na Halmashauri Kuu ya Wilaya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, Calisti Silayo amefariki dunia ghafla.
Silayo amefikwa na mauti baada ya kujisikia vibaya muda mfupi kabla ya kuanza kwa uchaguzi uliofanyika ukumbi wa Shauritanga, Ijumaa, Septemba 30,2022.
Katibu wa CCM Wilaya ya Rombo, Mary Sule amesema, muda mfupi kabla ya uchaguzi kuanza kwa wagombea kujieleza, Silayo alijisikia vibaya na kupelekwa Hospitali Teule ya Huruma kwa matibabu.
Via Mwananchi
Social Plugin