Mwanamke mmoja raia wa Congo ambaye aliolewa na waume wawili, amewaduwaza wengi ikizingatiwa kwamba ndoa ya waume wengi ni nadra barani Afrika.
Francine Jisele anaishi na waume wawili, mume wa kwanza Remi Murula na wa pili Albert Jarlace katika nyumba moja pamoja na wanao.
Jisele alifunga ndoa miaka sita iliyopita na Murula na walijaliwa watoto wawili. Murula aliondoka kwenda kutafuta kazi ya kukimu familia yake na kukata mawasiliano na mke wake.
"Kwa sababu maisha hayakuwa rahisi, mwanamume huyo alifunga safari na hakurudi tena. Nilijikuta pekee yangu, nilikaa miaka mitatu na nusu bila mume wangu," aliiambia Afrimax English katika mahojiano. "Baada ya miaka hiyo yote nilimpoteza na kupendana na mwanaume huyu mwingine.
Baada ya mwaka mmoja na mume wa pili, wa kwanza alirudi," alifichua. Jisele hakutarajia mume wake angerudi baada ya kuwa mbali kwa miaka yote hiyo.
“Nilikutana na mwanamke huyu nikiwa nafanya kazi kwenye sekta ya madini na akaniambia kuwa ana mume mwingine na jinsi mwanaume huyo alivyomuacha akisema anaenda kutafuta maisha,” “Nilihisi sina la kufanya kwa sababu tayari tulikuwa pamoja tangu nilipoishi naye bila kujua ana mwanaume mwingine,” alieleza Albert Jarlace.
“Mwanamke huyo aliniomba nisimuache hivyo nikaona ni lazima nibaki naye na kwa sasa tuna mtoto mmoja pamoja,” alisema Jarlace.
Murula aliporudi alipigana na Jarlace akibishana kuwa Jisele ni mke wake.
"Tuko wanaume watatu hapa na tunaelewana, huyu mwanamke ni mke wetu. Tangu niondoke sikuzungumza na mke wangu hata siku moja. Niliporudi nilimkuta mke wangu na mwanaume mwingine," aliongeza Murula.
Murula alikuwa amemwomba mpenzi wake amtimue Jarlace lakini alisisitiza kuwa hana mahali pengine pa kwenda.
"Mwanzoni nilipiga kelele lakini niligundua ikiwa ningezungumza na mke wangu hangefanya jambo kama hilo. Sikuwa na mahali pa kwenda na nilikuwa na makosa," alisema Murula.
“Tunakula meza moja, tunalala chumba kimoja na kitanda kimoja, nawapenda wote wawili, tunaishi kwa amani nyumbani,” alisema Jisele.
Wanaume hao hugawana kazi na kuleta mkate nyumbani huku mwanamke akiwaheshimu wote wawili. Wasiwasi walio nao ni kutoweza kuwatofautisha watoto wao. Mwanamke ndiye anayetambua baba wa watoto.
Wakati wa kusoma uroda
Linapokuja suala la kusoma uroda, mmoja wetu humwacha mwingine ili afurahie.
“Familia yangu inafahamu hali yangu na kunishauri nitulie kwa sababu nilimtelekeza mke wangu,” alisema Murula.
Jisele anasema ni ngumu kwake; anatamani kila mwanaume angekuwa na nyumba na angeenda kwao. Hataki wote watatu waendelee kukutana katika chumba kimoja cha kulala kwa wakati mmoja.
"Nataka kuondoka na kumpa nafasi 'hubby wa mwanamke huyo kwani ni mume wake anajulikana. Ningepata msaada wa tiketi ningeondoka na kumwacha mume mwenzangu abaki nyumbani kwake. Mwanamke asingekubali kuhama. mbali," alisema Jarlace.
"Sifurahii kuona sisi wanaume wawili tukigawana mwanamke; ardhi na nyumba ni yangu na mwanamke ni wangu," aliongeza.