JESHI la Polisi mkoani Songwe linamshikilia Nadi Saidi (60) Mkazi wa Kijiji cha Namkukwe wilayani Songwe kwa tuhuma za kumng'ata masikio hadi kumjeruhi mke wake Paulina Adam (20) aliyekuwa amemshika na kumvuta Mume wake huyo sehemu za siri baada ya kutokea ugomvi baina yao.
Kamanda wa Polisi mkoani humo Alex Mkama, amesema chanzo cha ugomvi wa wanandoa hao kilitokana na mwanaume kumlalamikia Mke wake baada ya kuuza mahindi debe moja bila ruhusa yake.
Baada ya malalamiko hayo ndipo ulitokea ugomvi ambapo mwanamke aliamua kushika sehemu za siri za mume wake kwa lengo la kujiokoa ambapo mume nae akiwa katika hatihati za kujinasua ndipo akaamua kumng'ata masikio yote mawili.
Mtuhumiwa tayari amefikishwa mahakamani kwa ajili ya kusomewa shtaka lake.
Social Plugin