Watoto 11 wamefariki dunia baada ya moto kuzuka katika shule ya watoto wasioona nchini Uganda.Watoto wengine wanne wako katika hali mahututi na wanatibiwa hospitalini.
Chanzo cha moto uliozuka jana katika shule ya bweni huko Mukono, mashariki mwa mji mkuu, Kampala, kinachunguzwa, lakini matukio kama hayo si ya kawaida.
Moja ya moto mbaya zaidi wa shule nchini humo ulikuwa katika shule ya Buddo Junior mwaka 2008 ambapo watoto kumi na tisa walifariki dunia.
Inasemekana kwamba kulikuwa na watoto wasiopungua 27 waliolala ndani ya bweni lililoathirika katika Shule ya iitwayo Salama .Wazazi waliokata tamaa wamekusanyika katika eneo hilo.
Matukio ya moto kwenye shule nchini humo yamekua yakisababishwa na watoto kutumia mishumaa katika mabweni yao.
Ripoti ya Jeshi la Polisi Machi mwaka huu ilieleza kuwa kumekuwa na matukio 18 ya moto shuleni katika kipindi cha miezi mitatu.