Mazishi ya aliyekuwa Mfanyabiashara na mwekezaji mzawa wa mkoa wa Shinyanga HilLal Hamad maarufu kwa jina la Phantom, yamefanyika leo Jumanne tarehe 04,10,2022, kwenye makaburi ya Waislamu yaliyopo Nguzonane katika Manispaa ya Shinyanga.
Mazishi ya Mwekezaji huyo ambaye pia alikuwa ni kada wa Chama cha Mapinduzi CCM, yamehudhuriwa na watu wa mbalimbali wakiwemo Wafanyabiashara ,Viongozi wa Serikali, na vyama vya siasa.
Akimzungumzia msiba huo, Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) Bwana Gasper Kileo , amesema marehemu Hillal ameacha pengo kubwa katika sekta ya uwekezaji na kwenye chama cha Mapinduzi na atakumbukwa kutokana na michango mbalimbali ya hali na mali aliyoitoa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Mabambasi uliopo Kata ya Ndembezi katika Mnispaa ya Shinyanga ambapo alikuwa akiishi Bwana Hillal enzi za uhai wake Bakari Khamis Juma, amemwelezea marehemu kuwa, licha ya kuwa na mwekezaji na mfanyabiashara mkubwa, alikuwa na mahusiano mazuri na jamii anayomzunguka ikiwemo kuchangia shughuli za maendeleo.
Bwana Hillal ambaye amewekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo ya mafuta, uchimbaji wa madini na elimu, amefariki dunia jana mchana jijini Dar es salaam, ambako alikuwa akipatiwa matibabu.
Chanzo- Radio Faraja
Social Plugin