RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kenya William Ruto ambapo pamoja na mambo mengine wamejadiliana namna ya kuendelea kudumisha uhusiano na ushirikiano kwenye mambo sita ya msingi.
Akizungumza leo Oktoba 10 katika Ikulu ya Dar es Salaam , Rais Samia amesema katika mazungumzo yao waliyofanya asubuhi wamejadiliana masuala mengi ya kimkakati yanayohusu uhusiano na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili kikanda na kimataifa.
Rais Samia amesema jambo la kwanza ambalo amezungumza na Rais Ruto kwenye mazungumzo yao kukuza ushirikianao na uhusiano wa nchi hizo mbili kama inavyoeleweka Tanzania na Kenya ukiacha mipaka ya kiuatawala mambo mengine wako wamoja.
“Tuna mpaka mkubwa lakini watu wetu wanashrikiana, watu wetu ni ndugu ,biashara zinakwenda mambo yetu ni mamoja kwa hiyo tumekubaliana kukuza na kuismarisha uhusiano,”amesema Rais Samia.
Amesema jambo la pili ni kuimarisha uhusiano wa kibiashara na kwamba kazi hiyo ilinza kati yake na Rais Uhuru Kenyata(Rais mstaafu) na walikubaliana kuwataka wataaalamu wao wafanyie kazi vikwazo vya biashara vilivyopo baina ya Kenya na Tanzania.
“Kwa ujumla watalaamu walitambua vikwazo 68 ambavyo vilifanyiwa kazi , vikwazo 54 viliondoka visivyo vya kikodi lakini bado kuna vikwazo 14 vimebakia.
“Tumewataka mawaziri wetu wa sekta ya bishara na uwekezaji wakutane haraka kufanyika kazi vikwazo 14 ili tuwe na uhuru mpana wa kufanya biashara lakini niseme kazi iliyoanza baina yetu Kenya na Tanzania kuondoa vikwazo imekuza sana biashara, mwenzangu Rais Ruto alikuwa anatoa takwimu.
“Akasema Tanzania mmefaidika mara mbili zaidi ya ilivyokuwa mnafaidika, kwa vikwazo vile vilivyoondolewa vimefaidisha lakini akasema ikifaidika Tanzania na Kenya imefaidika pia .Kenya na Tanzania tusigawane umasikini na udhalili lakini tugawane utajiri tutakaoufanya kupitia ufanyaji biashara.”
Aidha amesema jambo la tatu ni Mkutano wa nne wa Tume ya pamoja ya ushirikiano uliokuwa ufanyike Agosti mwaka huu lakini kwasababu ya mambo mengi haukufanyika , hivyo wamewataka mawaziri wao wakae wazungumze na kumaliza majadiliano haraka.
Rais Samia amesema jambo la nne wamezungumza na kukubaliana na Rais Ruto ni kuangalia mchakato wa kuimarisha mpaka wa kitaifa kati ya nchi hizo mbili kwani ni vema kuangalia mipaka kwasababu wanarithisha watoto wetu, hivyo wajue mipaka ya nchi zao imepita wapi ingawa kiutamaduni , kibinadamu hakuna mipaka lakini kuna mipaka ya kiuatala.
“Hivyo ni vema watoto wetu wajue mipaka imepita wapi na kazi hii katika awamu ya kwanza tumeifanya vizuri na sasa watalaamu wakakae kuangalia namna ya kuendesha mchakato huo awamu ya pili.”
Pia Rais Samia amesema wamezungumzia mradi wa bomba la kusafirsha gesi asilia kutoka Dar es Salaam hadi Mombasa ,mradi ambao walishasaini makubaliano pamoja na Rais Uhuru Kenyata lakini Rais Ruto ameubeba mradi uwe ndio mradi wake kwa kwanza atakaounza na Tanzania wa kusafirisha gesi dar es salaam kwenda Mombasa
Rais Samia amesema jambo lingine ambalo wamezungumza ni kushirikiana kudhibiti vitendo vya uhalifu unaovuka mipaka na hapo wamekubaliana na kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama kushirikiana kwa karibu, kuzungumza na kuangalia makosa yanayovuka mpaka.
“Uhalifu huo ni wa dawa za kulevya, uharamia , ujangili, pia masuala ya biashara ya kusafirisha watu.Tumewataka wakae waangalie nchi hizi mbili tutafanya vipi , wakati wanaosafirisha sio watanzania, sisi tunakamata tu lakini wakifika kwetu rekodi za dunia inaiona Tanzania au Kenya kwa hiyo inabidili tuangali vizuri,”amesema Rais Samia.
Pia wamejadiliana kuhusu kushirikiana katika Nyanja ya kikanda na kimataifa na hapo wamekubaliana kuendeleza ushirikiano mzuri na madhubuti kwenye Umoja wa Afrika pamoja na ushirikiano ndani ya Afrika Mashariki.
“Kwamba Kenya ,Tanzania na Uganda ndio viongozi wakubwa wa jumuiya hii, kwa hiyo hatuna budi kushirikiana ili wanaoungana nasi wakute kuna ushirikiano madhubuti uliojengwa nasi. Kwa ufupi hayo ndio tumezungumza kwenye mazungumzo yetu ya wawili lakini pia kwenye mazungumzo ya pamoja na watalaamu wetu.”.
Social Plugin