Mkurugenzi Mtendaji wa Samuu English Medium Pre and Primary School, Salome Samaytu akizungumza na wazazi na walezi.
***
Mahafali ya pili katika shule ya Awali na Msingi SAMUU ‘Samuu English Medium Pre and Primary School’ yamefanyika ambapo jumla ya wanafunzi 17 wamehitimu darasa la saba huku wanafunzi 31 wakihitimu shule ya awali ‘Nursery’ tayari kabisa kuanza masomo ya darasa la kwanza mwaka 2023.
Mahafali hayo yamefanyika leo Ijumaa Oktoba 28,2022 katika shule ya Msingi Samuu (Samuu English Medium Pre and Primary School) iliyopo katika kijiji cha Mwagala kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.
Akisoma Risala, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Awali na Msingi SAMUU, Moses Josiah amesema shule hiyo imeanzishwa Julai 13,2013 ikiwa na mwanafunzi mmoja na mwalimu mmoja ikiwa na madarasa mawili katika eneo la Ushirika Mjini Shinyanga na mwaka huu wanafunzi 17 wamehitimu elimu ya darasa la saba kati yao Wavulana ni 2 wasichana ni 15
“Kuanzia mwaka 2013 shule ya Samuu imekuwa ikifanya vizuri sana kitaaluma kwa kufanya vizuri kwenye mitihani ngazi ya mkoa na kitaifa ambapo kwa matokeo ya darasa la saba mwaka 2021 Shule ya msingi SAMUU ilishika nafasi ya kwanza Manispaa ,nafasi ya kwanza kimkoa na nafasi ya pili kitaifa na imefanikiwa kukuza vipaji mbalimbali vya watoto na sasa tuna zaidi ya wanafunzi 300 Tuna matarajio na mategemeo makubwa ya kufanya vizuri katika mtihani wa darasa la saba tuliofanya mwaka huu..Tuendelee kuombeana ili matokeo yawe mazuri sana kama tulivyotarajia”,amesema Josiah.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Samuu English Medium Pre and Primary School, Bi. Salome Samaytu amesema Shule hiyo kwa sasa inaendelea na mkakati wa kujenga uzio/ukuta katika eneo la shule ya Msingi SAMUU kituo cha Mwagala ili kuboresha hali ya usalama kwa wanafunzi wanao soma katika shule hiyo.
Amesema pia wanaendelea kukamilisha ujenzi wa bweni la watoto wa shule ya msingi hali itakayo saidia kuongeza kiwango cha taaluma shuleni hapo.
Aidha Mkurugenzi Samaytu amebainisha kuwa ili kubiresha kiwango cha elimu katika Shule ya Msingi SAMUU Shule ina mkakati wa kuanza kufundisha masomo ya lugha ya Kifaransa, Kichina na Kijerumani ili kuipandisha hadhi ya kuwa ya kimataifa (International school). Pia tuna mpango wa kuongeza safari za kimasomo ‘Study tour’ ili kuwajengea wanafunzi uwezo wa kujifunza kwa vitendo”,ameongeza Samaytu.
Mmiliki na Mkurugenzi wa SAMUU English Medium Pre and Primary School, Bw. Jonas Samaytu akitoa neno la shukrani amewashukuru wazazi na walezi kwa kuiamini shule hiyo na kupeleka watoto wao na kulipa ada huku akiwahimiza wazazi kulipa ada kwa wakati hali itakayo saidia kuendelea kuboresha miundo mbinu ya Shule hiyo.
Aidha amesema shule ipo kwenye mazingira na mandhari bora na wanafunzi hao waliohitimu elimu ya darasa saba wamewafundisha vizuri na wanaamini watafaulu vizuri katika mtihani wao wa taifa mwaka 2022 kama walivyofanya mwaka 2021.
Kwa upande wake Mgeni Rasmi katika mahafali hayo Shela Mshandete akimwakilisha Mstahiki Meya wamanispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko amesema serikali inatambua changamoto ya ya ukosefu wanishati ya umeme na kwamba tayari wamekwisha wasiliana na meneja watanesco kwa ajili ya kutatua changamoto ya umeme katika shule hiyo barabara na umeme katika shule hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Samuu English Medium Pre and Primary School, Salome Samaytu akizungumza kwenye mahafali.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Awali na Msingi SAMUU, Moses Josiah akisoma Risala mbele ya mgeni rasmi.
Wahitimu wa darasa la saba wakiendelea kutoa burudani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Samuu English Medium Pre and Primary School, Salome Samaytu akiongoza maandamano wakati wa mahafali
Mkurugenzi Mtendaji wa Samuu English Medium Pre and Primary School, Salome Samaytu akiongoza maandamano wakati wa mahafali
Wahitimu wa darasa la awali na darasa la saba katika mahafali ya pili .
Wazazi wa hitimu wakimsikiliza mgeni Rasmi.
Wazazi na walezi wakiwa makini kumsikiliza mgeni Rasmi.
Wazazi na walezi wakiwa makini kumsikiliza mgeni Rasmi.
Wazazi na walezi wakiwa makini kumsikiliza mgeni Rasmi.