Jeshi la Polisi limesema kuwa limeanza uchunguzi kuhusu malalamiko ya wananchi ya kutapeliwa fedha zao na kampuni ya Kalynda inayojishughulisha na biashara mtandao.
Taarifa iliyotolewa Jumamosi Oktoba 15, 2022 na Msemaji wa Jeshi hilo, David Misime imesema kuwa Ofisi Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai kwa kushiriana na taasisi nyingine za kiuchunguzi na za kifedha wameanza kuchunguza malalamiko hayo ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa.
Taarifa hiyo imesema, “Kutokana na malalamiko ya baadhi ya wananchi kulalamika kutapeliwa fedha zao na kampuni waliyoeleza ni Kalynda E Commerce kwa njia ya mtandao, Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai kwa kushiriana na taasisi nyingine za kiuchunguzi na za kifedha wameanza kuchunguza,” imesema taarifa hiyo.
Social Plugin