AfriMax kupitia ukurasa wao wa YouTube walisimulia kisa kimoja cha kushangaza kuhusu mwanaume mmoja ambaye ameoa wanawake 15 na ambaye bado anaazimia kuongeza wake zaidi.
Katika Makala hayo ambayo yalijikita upande wa Magharibi mwa Kenya ambapo walimtembelea mzee David Kaluhana mwenye umri wa miaka 62 ambaye amejizolea umaarufu kutokana na utajiri wake wa wanawake pamoja na watoto.
Kulingana na Makala hayo, Kaluhana mpaka sasa ni baba wa familia kubwa ya watoto 107 na ilisemekana kuwa nia na ndoto yake ni kufuata nyendo za mfalme Suleiman katika Biblia aliyekuwa na wanawake 700 na michepuko 300, jumla ya wanawake elfu moja.
Mzalishaji wa Makala hayo kwenye blogu ya YouTube ya AfriMax alisema kwamba mzee kaluhana kijijini kwao anatambulika kwa jina la kimajazi kama Genius kwa maana ya mtu mwenye akili zilizopitiliza.
Kaluhana alieleza kwamba kichwa chake mwanamke mmoja hawezi kukimudu na ndio maana anahakikisha kuwa na wanawake wengi kadri ya uwezo wake.
Kilichoshangaza wengi ni jinsi familia hiyo ilivyokuwa inaishi pamoja kwa Amani na upendo, kwa mbali mgeni atadhani ni watu wamejumuika pale kwa ajili ya mkutano au labda msiba kumbe ni familia ya baba mmoja – Mzee Kaluhana.
“Akili yangu ni kubwa sana, haiwezi kubebwa na bibi mmoja, akili yangu na bibi mmoja haviwezani, lakini kuwa na wake wengi unatakiwa kuwa na akili kubwa kwa sababu ukiwa huna akili kubwa hutaweza kuwaongoza,” mzee Kaluhana alimwambia mtayarishaji wa makala hayo aliyemsikiliza kwa mshangao mkubwa.
AfriMax waliweza kushuhudia jinsi familia hiyo inavyoshtaki njaa na katika kile kilichoonekana kama sinema, chai hutengenezwa kwa wingi na vitafunio hutawanyishwa kwa wingi ambapo familia hii yenye idadi sawa na shule inayoanza kujumuika nje kwa viti ambapo mzee huyo analishwa na kuchungwa kama mfalme na heshima zake za kudumu.
Aidha mzee huyo aliteua kitendawili cha lishe kwa familia yake ambapo alisema yeye ni riziki yake ni kutokana na weledi wake katika historia. Alisema kuwa huwa anapewa mialiko katika mataifa jirani kusimulia matukio mbali mbali ya kizamani na haapo ndipo riziki yake hujipa kwa ajili ya kuilisha familia yake kubwa.
Kama haya si maajabu basi ni miujiza!