Vijana wawili waliojulikana kwa majina ya Ibrahimu Shaban (21) na Mussa Bakari (28) wamefariki dunia baada ya kupigana kwa kutumia magongo ya miti wakigombea mpenzi aitwaye Hadija Msamati katika kijiji cha Mkangaula kata ya Namalenga wilayani Masasi mkoani Mtwara.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo amesema watu wawili wamefairiki dunia kwenye ugomvi wa kupigana wao kwa wao wakigombea mwanamke wilayani Masasi Septemba 29, 2022 majira ya saa sita usiku.
Kamanda Matembo amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara linamtafuta Hadija Msamati kwa mahojiano akidaiwa kuhusika katika vifo hivyo baada ya ugomvi huo kwani mwanamke huyo amekimbilia kusikojulikana baada ya tukio hilo.
"Chanzo cha tukio hili ni wivu wa mapenzi. Kwa mujibu wa taarifa ya Daktari baada ya uchunguzi walibaini chanzo ni kuvuja damu kwa wingi mwilini", amesema Kamanda Katembo.
Social Plugin