Katika hali ya kushangaza watu wasiojulikana wamevamia nyumba ya mzee wa miaka 70, Uruban Paul mkazi wa kijiji cha Urushimbwe mkoani Kilimanjaro kisha kumkata sehemu zake za siri.
Akielezea tukio hilo lililotokea usiku wa Oktoba 16, mzee huyo amesimulia kuwa siku hiyo alikuwa akitoka kwenda kujisaidia na ndipo alipokutana na watu hao ambao anadai kuwa baada ya kumfanyia ukatili huo walikuwa wakikinga damu yake.
“Wakati natoka ndani kwenda kujisaidia usiku ghafla nikavamiwa na watu walionikaba na kunifunga na kitu usoni nisione, wakaniingiza ndani wakanivua nguo na wakati huo nilikuwa siwezi kupiga ukunga kuomba msaada kwa majirani zangu, walinilaza chini wakaanza kunikata sehemu ya uume wangu, nilipata maumivu makali sana,” amesimulia.
Aidha, Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Alexanda Temba amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusikitishwa na ukatili uliofanyika kwa mzee huyo.
Mzee huyo ameiomba Serikali imsaidie ili waliofanya tukio hilo la ukatili waweze kukamatwa na kufikishwa mahakamani.
Via: ST
Social Plugin