Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BENKI YA EXIM YAKABIDHI MSAADA WA MADAWATI 100 TANGA

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw Omary Mgumba (wanne kulia) akipokea msaada wa madawati 100 kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Tanzania Bw Jaffari Matundu (watatu kushoto) ikiwa ni jitihada za benki hiyo katika kuboresha elimu mkoani humo wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ofisi ya Mkuu wa mkoa hii leo. Wanaoshuhudia ni pamoja na Katibu Tawala Mkuo huo Bi Pili Mnyema (Kulia), Afisa Elimu Mkoa wa Tanga Bi Newaho Mkisi na baadhi ya maofisa waandamizi wa mkoa huo pamoja benki ya Exim. Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw Omary Mgumba (katikati walioketi)) sambamba Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Tanzania Bw Jaffari Matundu (kushoto walioketi) na Katibu Tawala Mkuo huo Bi Pili Mnyema (Kulia walioketi) wakijaribu ubora wa madawati yaliyotolewa na Benki ya Exim ikiwa ni jitihada za benki hiyo katika kuboresha elimu mkoani humo wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ofisi ya Mkuu wa mkoa hii leo. Wanaoshuhudia ni pamoja na Afisa Elimu Mkoa wa Tanga Bi Newaho Mkisi (wa tatu kulia) na baadhi ya maofisa waandamizi wa mkoa huo pamoja benki ya Exim. Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw Omary Mgumba (watatu kulia) akikabidhi msaada wa madawati 100 yaliyotolewa na Benki ya Exim kwa Katibu Tawala Mkuo huo Bi Pili Mnyema ikiwa ni jitihada za benki hiyo katika kuboresha elimu mkoani humo wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ofisi ya Mkuu wa mkoa hii leo. Wanaoshuhudia ni pamoja na Afisa Elimu Mkoa wa Tanga Bi Newaho Mkisi (Kulia) na baadhi ya maofisa waandamizi wa mkoa huo pamoja benki ya Exim. Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Bi Pili Mnyema (wa pili kushoto) akikabidhi msaada wa madawati 100 yaliyotolewa na Benki ya Exim kwa Afisa Elimu Mkoa wa Tanga Bi Newaho Mkisi ikiwa ni jitihada za benki hiyo katika kuboresha elimu mkoani humo wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ofisi ya Mkuu wa mkoa hii leo. Wanaoshuhudia ni baadhi ya maofisa waandamizi wa mkoa huo pamoja benki ya Exim. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Tanzania Bw Jaffari Matundu (wa pili kushoto) akimkabidhi zawadi maalum Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw Omary Mgumba ikiwa ni ishara ya benki hiyo kutambua jitihada zake katika kuendeleza mkoa huo wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya madawati 100 yaliyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya mkoa wa Tanga iliyofanyika kwenye ofisi ya Mkuu wa mkoa hii leo. Wanaoshuhudia ni maofisa waandamizi wa mkoa huo pamoja benki ya Exim. Akizungumza mara baada ya kupokea msaada wa madawati 100 yaliyotolewa na Benki ya Exim kwa ajili ya mkoa huo mapema leo jijini humo, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw Omary Mgumba (pichani) pamoja na kuonesha kuvutiwa zaidi na ubora wa madawati hayo alisema msaada huo umekuja wakati muafaka kwa kuwa mkoa huo kwasasa upo kwenye mpango mahususi wa kukabiliana na changamoto kubwa ya uhaba wa madawati inayoukabili mkoa huo. Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Bw Jaffari Matundu (pichani) alisema msaada huo ni sehemu ya hitimisho la kampeni ya ugawaji wa madawati 1000 iliyozinduliwa mwishoni mwa mwaka jana Waziri Mkuu Kassim Majiliwa ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwa benki hiyo. Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw Omary Mgumba (wanne kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na maofisa waandamizi wa benki ya Exim wakiongozwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Bw Jaffari Matundu (wanne kulia) pamoja na maofisa waandamizi wa mkoa huo akiwemo Katibu Tawala Mkuo huo Bi Pili Mnyema ( wa tatu kulia) na Afisa Elimu Mkoa wa Tanga Bi Newaho Mkisi ( wa pili kulia) wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya madawati 100 yaliyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya mkoa wa Tanga iliyofanyika kwenye ofisi ya Mkuu wa mkoa hii leo. .................................. Na Mwandishi Wetu-TANGA Ikiwa inaelekea ukiongoni, kampeni ya ugawaji wa madawati 1000 inayoendeshwa na benki ya Exim Tanzania katika mikoa mbalimbali hapa nchini imeonesha mafanikio makubwa huku ubora wa madawati hayo ukionyesha kuwavutia wakuu wa mikoa waliopokea msaada huo akiwemo mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw Omary Mgumba. Akizungumza mara baada ya kupokea msaada wa madawati 100 yaliyotolewa na Benki ya Exim kwa ajili ya mkoa huo mapema hii leo jijini humo, Bw Mgumba pamoja na kuonesha kuvutiwa zaidi na ubora wa madawati hayo alisema msaada huo umekuja wakati muafaka kwa kuwa mkoa huo kwasasa upo kwenye mpango mahususi wa kukabiliana na changamoto kubwa ya uhaba wa madawati inayoukabili mkoa huo. “Changamoto ya madawati katika mkoa wa Tanga ni kubwa licha ya jitihada tunazoendelea kuzifanya. Wilaya pekee yenye auheni ni wilaya ya Pangani yenye uhaba wa madawati 400 huku wilaya ambayo inaongoza kwa uhaba wa mkubwa wa madawati katika mkoa huu ni Lushoto ikiwa na uhaba wa madawati 1500 na hiyo ni kwa shule za msingi pekee. Hivyo tunawashukuru sana Benki ya Exim kwa msaada huu wa madawati ambayo ni bora zaidi’ Alisema Bw Mgumba. Aidha RC Mgumba, alitoa wito kwa wadau mbalimbali mkoani humo kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu katika kuleta maendeleo katika nyanja mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu na afya kupitia mipango yao uwajibikaji kwa jamii. “Tukimsaidia vema Mh Rais kupitia jitihada kama hizi zilizofanywa na benki ya Exim tafsiri yake pia hata kasi ya maendeleo inaongezaka kwasababu nguvu ambazo zingetumiwa na Mh Rais na serikali kwa ujumla katika ununuzi wa madawati zinaelekezwa kwenye mipango mingine ya kimaendeleo ikiwemo ujenzi wa madarasa na hivyo tunajikuta tunaharakisha maendeleo,’’ alisema Bw Mgumba. Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Bw Jaffari Matundu alisema msaada huo ni sehemu ya hitimisho la kampeni ya ugawaji wa madawati 1000 iliyozinduliwa mwishoni mwa mwaka jana Waziri Mkuu Kassim Majiliwa ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwa benki hiyo. “Msaada huu wa madawati 100 hapa mkoani Tanga unaashiria mwanzo wa hitimisho la kampeni yetu ya ugawaji wa madawati 1000 iliyofanyika kwa mafanikio makubwa kutokana na ukweli kwamba mikoa yote ambayo tumekabidhi msaada huu ilionyesha kuvutiwa na ubora wa madawati haya yaliyotengenezwa kwa ubora wa hali ya juu ili yaweze kutumika kwa muda mrefu,’’ alisema. Aliitaja baadhi ya mikoa ambayo tayari imenufaika na msaada huo kuwa ni pamoja na Dodoma, Mwanza, Lindi, Mbeya, Mtwara, Tabora, Shinyanga na Tanga. Akizungumzia msaada huo Afisa Elimu Mkoa wa Tanga Bi Newaho Mkisi pamoja na kuishukuru benki ya Exim kwa msaada huo alisema utasaidia kupunguza changamoto ya uhaba wa madawati katika baadhi ya shule zilizopo wilayani humo ambazo kwasasa zinakabiliwa na uhaba mkubwa wa madawati unaotokana na ongezeko la vyumba vya madarasa kufuatia ujenzi wa vyumba hivyo unaoendelea kutelekelezwa na serikali katika maeneo mbalimbali mkoani humo. Bi Mkisi alitoa wito kwa walimu na wanafunzi watakaonufaika na msaada huo kutunza madawati hayo ili yaweze kutumika kwa muda mrefu na hivyo kusaidia walengwa wengi zaidi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com