Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jaffo (kushoto) akizungumza na Kaimu Meneja wa PSSSF Mkoa wa Geita Bw. Kiwamba Saidi (kulia) wakati Waziri huyo alipotembelea katika Banda la Mfuko huo katika Maonesho ya tano ya Sekta ya Madini yanayofanyika katika viwanja vya Bombambili EPZA Geita.
Waziri Jaffo amekuwa mgeni rasmi wa siku ya leo Oktoba 6,2022 ambapo ameiagiza PSSSF kuweka vifaa maalum vya kutunzia taka (Dustbins) katika maeneo mbalimbali nchini kwa namna ambavyo PSSSF watapendekeza ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya 6 ya Rais Samia Suluhu Hassan ya utunzaji wa Mazingira.
Aidha Waziri Jaffo ameipongeza PSSSF kwa kazi nzuri wanayofanya ya kulipa mafao kwa wakati na kuwawezesha wastaafu kuwa na uhakika wa maisha yao baada ya kustaafu.
(Picha Na: Hughes Dugilo)
Kaimu Meneja wa PSSSF Mkoa wa Geita Bw. Kiwamba Saidi (kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jaffo (kushoto) alipofika kwenye Banda la Mfuko huo kujionea shughuli wanazozifanya katika Maonesho ya Madini Geita.
Kaimu Meneja wa PSSSF Mkoa wa Geita Bw. Kiwamba Saidi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Mfuko huo katika Banda lao.
Social Plugin