Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Taifa ,Abdulrahman Kinana (wa tatu kulia) akiwa na viongozi Waandamizi wa Taaisis na Shule ya Mwalimu Nyerere pamoja na Wageni waalikwa wakifuatilia mijadala iliyokuwa ikitolewa ukumbini humo mara baada ya ufunguzi wa mdahalo wa kumbukizi ya miaka 23 ya Mwalimu Julius Nyerere,ulioandaliwa na Taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere kwa kushirikiana na shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere,Oktoba 12,2022 Kwamfipa Kibaha Mkoani Pwani.PICHA ZOTE NA MICHUZI JR- KIBAHA PWANI.
Na Mwandishi Wetu,Kibaha
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana ametaja mambo manne ambayo Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alikuwa akiyasimamia enzi ya uhai wake kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania.
Kinana ameyataja mambo hayo leo Oktoba 12, 2022 wilayani Kibaha mkoani Pwani wakati wa mdahalo kuelekea kumbukizi ya miaka 23 ya hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Akifungua Mdahalo huo Uliofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere, Uliokutanisha vyama rafiki vya ukombozi Kusini mwa Afrika, Viongozi mbalimbali pamoja na Wanazuoni, Kinana amesema falsafa ya Mwalimu Nyerere ilijengwa na misingi imara kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania na Bara la Afrika kwa Ujumla.
" Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere alikuwa na maono ya kujua Uelekeo wa Taifa na Wapi Watanzania wanatakiwa kuelekea na hiyo ilitokana na Msimamo wake na kutotetereka," amesema Kinana.
Kuhusu suala la Uadilifu, Kinana amesema Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere alikuwa na misingi ya uadilifu na kwa kujali aliokuwa akiwaongoza ambapo alipenda Uongozi Shirikishi.
"Pia Mwalimu Nyerere alikuwa na Ushawishi mzuri kwenye Chama na Serikali na hiyo ilisababishwa na uwezo wake mkubwa wa Kujenga hoja kwa ajili ya maslahi ya aliokuwa akiwaongoza," amesisitiza Kinana.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Paul Kimiti ameomba watanzania kuyaendeleza yale yote mema yaliyofanywa na mwalimu ili kulijenga taifa katika misingi imara ya upendo mshikamano na umoja zaidi.
Wakati huo huo Mkuu wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Profesa Maselino Chijoliga amewakaribisha viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali kwenda kusoma kozi fupi za uongozi zilizopo katika chuo hicho ili ziwajengee uwezo wa kuongoza vyema kwa maadili ya uzalendo.
Katika hatua nyingine Taasisi ya Mwalimu Nyerere imemkabidhi Komredi Kinana Katiba na Hati ya Usajili wa Taasisi hiyo pamoja Vipeperushi vinayoelezea Historia ya Mwalimu Nyerere kwa Ujumla.
Oktoba 14 mwaka huu itakuwa ni kumbukizi ya miaka 23 ya hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere tangu alipoaga Dunia. Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Taifa ,Abdulrahman Kinana akizungumza jana Oktoba 12,2022 wakati akifungua mdahalo wa kumbukizi ya miaka 23 ya Mwalimu Julius Nyerere,ulioandaliwa na Taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere kwa kushirikiana na shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kwamfipa Kibaha Mkoani Pwani.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Paulo Kimiti akimkabidhi Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Taifa ,Abdulrahman Kinana Katiba na Hati ya Usajili wa Taasisi hiyo pamoja na Vipeperushi vinayoelezea Historia ya Mwalimu Nyerere kwa Ujumla mara baada ya kufungua mdahalo wa kumbukizi ya miaka 23 ya Mwalimu Julius Nyerere,ulioandaliwa na Taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere kwa kushirikiana na shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere,Oktoba 12,2022 Kwamfipa Kibaha Mkoani Pwani.
Wageni waalikwa wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini hummo katika mdahalo wa kumbukizi ya miaka 23 ya Mwalimu Julius Nyerere,ulioandaliwa na Taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere kwa kushirikiana na shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere,Okotoba 12,2022 Kwamfipa Kibaha Mkoani Pwani. PICHA ZOTE NA MICHUZI JR- KIBAHA PWANI. Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Taifa ,Abdulrahman Kinana wa tatu kulia akiwa ameambatana na Viongozi Waandamizi wa Taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere na Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere sambamba na Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani (kulia) Mhe.Abbubakar Kunenge akielekea ukumbini kwa ajli ya kufungua mdahalo wa kumbukizi ya miaka 23 ya Mwalimu Julius Nyerere,ulioandaliwa na Taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere kwa kushirikiana na shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere jana Oktoba 12,2022 Kwamfipa Kibaha Mkoani Pwani. Muonekano wa Jukwaa kuu Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Taifa ,Abdulrahman Kinana akiwasili kwenye jukwaa kuu jana Oktoba 12,2022 kwa ajili ya kufungua mdahalo wa kumbukizi ya miaka 23 ya Mwalimu Julius Nyerere,ulioandaliwa na Taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere kwa kushirikiana na shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kwamfipa Kibaha Mkoani Pwani.PICHA ZOTE NA MICHUZI JR- KIBAHA PWANI. Baadhi ya Wakuu wa Wilaya mkoa wa Pwani wakishiriki ufunguzi wa Mdahalo huo
Mkuu wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Prof Marcelina Chijoriga akiwakaribisha viongozi wa Jukwaa na Kuu na Wageni waalikwa mbalimbali waliofika kuhudhuria ufunguzi wa mdahalo wa kumbukizi ya miaka 23 ya Mwalimu Julius Nyerere,ulioandaliwa na Taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere kwa kushirikiana na shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kwamfipa Kibaha Mkoani Pwani. Wachokoza Mada wa Mdahalo huo,pichani kulia ni aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndg Wilson Mukama,Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dkt Ayub Rioba,Mkuu wa Utawala wa CCM OND-Lumumba Christopher Ngubiagai pamoja na Aliyewahi kushika Nyadhifa mbalimbali za Uwaziri nchini Mhe.Fatma Said Ally Mchuno
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Paulo akitoa utambulisho na neno la kumkaribisha rasmi Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Taifa ,Komredi Abdulrahman Kinana kwa ajili ya ufunguzi wa mdahalo wa kumbukizi ya miaka 23 ya Mwalimu Julius Nyerere,ulioandaliwa na Taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere kwa kushirikiana na shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere,Oktoba 12,2022 Kwamfipa Kibaha Mkoani Pwani. Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Taifa ,Abdulrahman Kinana akizungumza jana Oktoba 12,2022 akisisitiza jambo wakati akifungua mdahalo wa kumbukizi ya miaka 23 ya Mwalimu Julius Nyerere,ulioandaliwa na Taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere kwa kushirikiana na shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kwamfipa Kibaha Mkoani Pwani.
Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi Wilson Mukama akieleza mada iliyohusu Mchango wa Mwalimu Nyerere katika Uongozi wa Chama wakati wa mdahalo wa kumbukizi ya miaka 23 ya Mwalimu Julius Nyerere,ulioandaliwa na Taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere kwa kushirikiana na shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kwamfipa Kibaha Mkoani Pwani.
Picha mbalimbali juu zikiomuonesha Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Taifa ,Abdulrahman Kinana akisalimiana na Viongozi Waandamizi wa Taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere na Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere mara baada ya kuwasili jana Oktoba 12,2022 kwa ajili ya
kufungua mdahalo wa kumbukizi ya miaka 23 ya Mwalimu Julius Nyerere,ulioandaliwa na Taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere kwa kushirikiana na shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kwamfipa Kibaha Mkoani Pwani.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Taifa ,Abdulrahman Kinana alipokelewa pia na Gwaride la heshima kuoka kwa Vijana wa CCM mara baada ya kupokewa na Viongozi Waandamizi wa Taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere na Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere kwa ajli ya kufungua mdahalo wa kumbukizi ya miaka 23 ya Mwalimu Julius Nyerere,ulioandaliwa na Taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere kwa kushirikiana na shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kwamfipa Kibaha Mkoani Pwani.PICHA ZOTE NA MICHUZI JR- KIBAHA PWANI.
Social Plugin