Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ACHOMWA KWA UJI WA MOTO KISA KULA MAHARAGE KIJIKO KIMOJA BILA RUHUSA


Mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Violet Masawe mkazi wa mtaa wa Bogini Wilayani Moshi Mkoani Kilimanjaro anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumchoma kwa uji wa moto mtoto wa kaka yake aliyetambulika kwa jina la Elvis Shoo mwenye umri wa miaka 27.


Inaelezwa kuwa kuwa Kijana Elivis alichukua kijiko cha maharage na kula pasipo kumhusisha shangazi yake ndipo yalipotokea majibizano yaliyopelekea kijana huyo kumwagiwa uji wa moto tukio ambalo limemsababishia kupata Majeraha katika Maeneo ya mwili wake ikiwemo eneo la shingoni na hivi sasa amelazwa katika hospitali ya Pasua mjini Moshi kwaajili ya kupatiwa Matibabu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com