Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt.Selemani Jafo amesema ni vema suala la upandaji miti katika nchi yetu liwe endelevu ili kusaidia kuhifadhi mazingira.
Jafo aliyasema hayo leo Oktoba 23,2022 baada ya kuongoza upandaji miti uliofanyika katika Shule ya Msingi Mtoni wilayani Bagamoyo mkoani Pwani na kuratibiwa na benki ya Standard Chartered ambapo amewahimiza wananchi kuendelea kuhamasisha kupanda miti.
"Upandaji wa miti kwa wingi kwenye mazingira ni njia mojawapo itakayosaidia kukabiliana na changamoto ya hewa ukaa inayoweza kuhatarisha maisha ya mwanadam",alisema Japo.
Jafo ameipongeza Benki ya Standard Chartered kwa kumualika katika zoezi la upandaji miti katika shule hiyo na kwamba ameomba taasisi za Serikali na binafsi nchini kuiga mfano wa Benki ya Standard Chartered kwa hatua ya kuleta miche ya miti 1000
Amesema ajenda ya mazingira ndiyo ajenda inayosababisha uchumi kuwa imara,lakini pia akawataka wanafunzi kupeleka ujumbe kwa wazazi wao kushiriki zoezi zima la kupanda Miti katika maeneo yao.
"Serikali imekuwa na mikakati mbalimbali katika kuhakikisha inatunza mazingira ili kuwa na mazingira safi,na miongoni mwa mikakati hiyo ni upandaji miti katika taasisi za serikali na binafsi nchini,"amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Herman Kasekende amesema amefarijika sana kuona watanzania wanapanda miti kwa wingi.
"Benki yetu ya Standard Chartered itaendelea kuunga mkono juhudi mbalimbali za upandaji miti na kuhakikisha Tanzania inakua ya kijani kama maelekezo ya Serikari ya kupanda miti katika maeneo yote nchi nzima,
Kwa hiyo na sisi pamoja na Waziri Jafo tunashiriki kupanda Miti Elfu moja (1000) katika shule hii katika hatua ya kupambana na mabadiliko tabianchi na kutunza Mazingira",alisema
Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dk. Seleman Jaffo (katikati), akipanda mmoja ya miti 1000 iliyotolewa na Benki ya Standard Chartered iliyopandwa katika Shule ya Msingi Mtoni Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani na (kushoto) ni Afisa Tawala wa Wilaya Magamoyo, Casilda Mgeni, na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Herman Kasekende.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Herman Kasekende akipanda mti huku Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt.Selemani Jafo akishuhidia katika Shule ya Msingi Mtoni Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani jana tarehe 22 Oktoba 2022.iliyotolewa na benki ya Standard Chartered.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt.Selemani Jafo akishuhudia Viongozi wa CCM Wilaya Bagamoyo Mkoa wa Pwani wakipanda mti kwenye shule hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akikabidhiwa fulana kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Herman Kasekende kushoto ni Afisa Tawala Wilaya Bagamoyo mkoa wa Pwani, Casilda Mgeni.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo,akihutubia wadau mbalimbali wa Mazingira wakati wa upandaji miti Elfu moja (1000) iliyotolewa na Benki ya Standard Chartered na kupanda katika Shule ya Msingi Mtoni Wilaya ya
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Herman Kasekende akisoma hotuba yake wakati wa upandaji miti Elfu moja (1000) iliyotolewa na Benki hiyo iliyopandwa leo Oktoba 23,2022 katika Shule ya Msingi Mtoni Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani. (PICHA ZOTE EMMANUEL MASSAKA WA MICHUZI TV)
Wadau mabalimbali wa Mazingira wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo (hayupo pichani)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani tarehe 22 Oktoba 2022.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa CCM Wilaya Bagamoyo Mkoa wa Pwani jana tarehe 22 Oktoba 2022.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Shule ya Msingi Mtoni Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Sehemu ya Mti .(PICHA ZOTE EMMANUEL MASSAKA WA MICHUZI TV)
Social Plugin