MAAFISA UHAMIAJI WAUAWA KWA KUPIGWA MISHALE GEITA

 



Maofisa wa Idara ya Uhamiaji wawili wa Wilaya ya Bukombe mkoani Geita wameuawa kwa kupigwa mishale na wananchi wa kijiji cha Mtakuja Kata ya Lulembela Wilaya ya Mbogwe.


Maofisa hao waliofahamika kwa jina moja; Salum na Mtobi wameuawa usiku wa kuamkia leo Jumatano Oktoba 26.


Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Geita, Emmanuel Lukumay amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ingawa hakutaja sababu za mauaji hayo huku akiahidi kutoa taarifa zaidi baada ya kufika eneo la tukio.


“Nimepata taarifa hizo na hivi sasa niko njiani naenda eneo la tukio. Hadi sasa bado hatujajua sababu za mauaji hayo. Nitatoa taarifa zaidi baada ya kufika huko,” amesema Lukumay


Habari zilizopatikana kutoka kijiji cha Mtakujaa zinasema kuwa maofisa hao waliuawa usiku wa kuamkia leo baada ya kufika kijijini hapo kwa lengo la kuwakamata watu wanaodaiwa kuwa ni wahamiaji haramu ambao walikuwa nyumbani kwa mkazi wa kijiji hicho.


CHANZO - MWANANCHI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post