Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JK NA WAZIRI MKUU WA CANADA


Rais Mstaafu Jakaya Kikwete amekutana na Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau katika hafla ya mchapalo iliyofanyika Ottawa, Canada. 

Katika mazungumzo mafupi waliyofanya Rais Mstaafu Kikwete ameishukuru Canada kwa kuendeleza mahusiano mazuri yaliyodumu kwa muda mrefu kati ya Canada na Tanzania hususan katika eneo la uwekezaji na ufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania. 

Waziri Mkuu Trudeau amemshukuru Rais Mstaafu Kikwete kwa kuhudhuria hafla hiyo iliyoandaliwa kwa heshima ya Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC), Moussa Faki Mahamat na kumweleza namna anavyothamini kwa dhati mahusiano baina ya nchi hizo mbili na kuahidi kuendelea kuyadumisha. 

Aidha, alimdokeza kuwa bado ana kumbukumbu nzuri za kuitembelea Tanzania Mwaka 1981 (yeye kavaa singleti nyeupe) wakati Baba yake Pierre Trudeau akiwa Waziri Mkuu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com