Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TANZANITE SUPPORT ORGANIZATION (TSO) YAENDELEA KUTOA ELIMU NA MAFUNZO MBALIMBALI KWA VIJANA


Tanzanite Support Organization (TSO), ni Taasisi isiyo ya Kiserikali yenye makao yake makuu Mikocheni Dar es Salaam, Tanzania.


Shirika la Tanzanite Support linatoa msaada kwa makundi ya vijana kwa kuwapatia elimu na ujuzi katika fani mbalimbali.

TSO tumedhamiria kubadilisha maisha ya vijana na kuwasaidia kufikia malengo yao na kujitegemea, Kuwashawishi wao binafsi kufanya vyema, kuwa makini zaidi na nafasi zao katika nyanja zote za maisha na kazi, kwa kuwapatia taarifa, uwezeshaji, ukuzaji, ujuzi, huku ukitoa nyenzo muhimu na ushauri.

Lengo hasa ni kundi la watu ambao wako katika hali na mazingira yaliyoathiriwa hasa vijana, wanawake na watoto. Kwa vijana juhudi zetu ni kwa wale walio katika nyumba za kulea watoto na ambao hawawezi tena kuhudumiwa katika vituo hivi baada ya kufikia umri wa miaka 18. Lengo ni kuwawezesha kujisimamia wenyewe baada ya kuondoka kwenye vituo vyao. Tunafanya hivi kupitia elimu na uwezeshaji wa kiuchumi. Tunawaingiza katika programu yetu ya “Achieving Self-Reliance” (ASR) ambayo inawatayarisha kutekeleza malengo yao. Tunafanya kazi haswa na vijana wenye umri wa miaka 15-18 kwa mpango huu.

Tunafanya kazi na wadau mbalimbali katika hatua zote za programu zetu. Vituo vya kulea watoto na mashirika mengine ambayo yanaweza kufikia vijana wanaoishi katika mazingira magumu. Tunawaleta katika kituo chetu na kuwapatia mafunzo, na kozi za kujiandaa kwa maisha ikijumuisha afya ya akili.

Katika kila hatua tunafanya kazi na washirika ambao aidha, hutoa huduma kama vile mafunzo ya kujitolea, mpango wa stadi za maisha na matokeo yake ni kuwapatia mafunzo ya kazi na ajira ambayo TSO inafuatilia ili kuhakikisha walengwa wanaishi maisha yenye mafanikio na kutimiza malengo yao.

Mazoezi ya viungo (YOGA)
Bi. Sumaiya Mahmoud kutoka Mind Garden akiwafundisha vijana Elimu kuhusu Afya ya akili. Mind Garden wanatoa huduma mbalimbali katika masuala ya kitabia, kihisia, kisaikolojia na akili kwa watu wote wakiwemo watoto, vijana na watu wazima.
Vijana kutoka TSO - Tanzanite Support Organization wakiwa pamoja na Dr. Sylvia akiwafundisha Elimu ya Afya ya Uzazi na Hedhi salama. Faida za kupata elimu ya afya ya uzazi ni pamoja na: -Kuepuka mimba za utotoni -Kuepuka changamoto za uzazi -Kuepuka ndoa za utotoni na pia kuepuka kupata maambukizi ya magonjwa ya zinaa, etc

Bw. Rahim kutoka UTT Amis akitoa Elimu ya maswala ya Fedha na Uchumi kwa vijana wanaopatiwa mafunzo ya kujiendeleza katika shirika la Tanzanite support organization (TSO) Kampuni ya UTT AMIS inasimamia Mifuko sita ya uwekezaji wa pamoja ambayo ni Mfuko wa Umoja, Mfuko wa Wekeza Maisha, Mfuko wa Watoto, Mfuko wa Kujikimu
Vijana wakifurahia jambo kwa pamoja wakati wakipata mafunzo

Bw. Beda Shayo kutoka kampuni ya Ahava Security Group (ASG) akizungumza na vijana na kuwapa mafunzo namna kampuni hiyo inavyofanya kazi. Baadhi ya vijana wameshaajiriwa katika kampuni hiyo ya Ahava security na wanaendelea na majukumu yao.
Vijana wakiwa Katika picha ya pamoja na bi. Sumaiya Mahmoud kutoka Mind Garden

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com