Takribani watu 76 wameripotiwa kupoteza maisha baada ya boti waliyokua wamepanda kupata ajali huko Kusini Mashariki mwa jimbo la Anambra nchini Nigeria.
Boti hiyo ambayo ilikua imebeba takribani watu 80 , ilizama siku ya Ijumaa katika eneo la Ogbaru jimbo la Anambra.
Waathirika wakubwa kwenye ajali hiyo ni wanawake na watoto ambao walikua wakitafuta usalama wa maisha yao baada ya mafuriko makubwa kuikumba jamii yao.
Rais wa Nigera Muhammadu Buhari ametoa salamu zake za rambirambi kufuatia tukio hilo akiliita kuwa janga kubwa.
Pia ametaka kufanywa kwa uchunguzi wa usalama wa usafiri wa majini nchini humo na kwamba vikosi vya dharura vifanye kila kinachowezekana kuwatafuta waliopotea
Social Plugin