Mwanamke aliyejifungua watoto tisa
MWANAMKE mmoja mwenye umri wa miaka 35 aliyefahamika kwa jina la Hajara Shu’aibu, amekuwa na kila sababu ya kutabasamu baaada ya kujaliwa kupata watoto 9 mapacha.
Mwanamke huyo anayeishi jimbo la Katsina nchini Nigeria alijifungua watoto hao Jumatano ya wiki iliyopita, Oktoba 5, 2022 na sasa ana jumla ya watoto 18. Hajara tayari alikuwa na alikuwa na watoto wengine tisa mapacha ambao aliwahi kujifungua miaka kadhaa iliyopita na wote wapo hai.
Mama huyu ambaye anaonekana kama mama aliyebarikiwa na zawadi ya watoto kwenye jamii yao, ameolewa na mkulima miaka 21 iliyopita.
“Nilijifungua nikiwa nyumbani, baadaye wakunga walinipeleka hospitalini na kuwekwa damu kisha kuniambia nipumzike. Watoto wangu wote waliozaliwa hapo awali wapo nyumbani. Watoto wangu wote nilijifungulia nyumbani bila upasuaji hata mmoja,” mama alisema.
Akizungumza kuhusu kujifungua kwake hivi majuzi, mama huyo alisema watoto hao wachanga walipelekwa katika Hospitali Kuu ya Funtua iliyoko karibu baada ya kujifungulia nyumbani.
Hata hivyo mama huyu alitoa wito kwa serikali na watu binafsi wenye moyo wa huruma kumsaidia kuwatunza watoto.
Social Plugin