Wajumbe wa Kamati ya ukusanyaji mapato ya ndani halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mradi wa machinjio ya kisasa Ndembezi ambao pia una mchango wa fedha za mapato ya ndani.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
KAMATI ya ukusanyaji mapato ya ndani halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, wameipongeza manispaa hiyo kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo itokanayo na fedha za makusanyo ya mapato ya ndani.
Katibu wa Kamati hiyo Dk. Kulwa Meshack, akizungumza kwenye ziara hiyo, amesema wamefanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo Manispaa ya Shinyanga, ili kuona fedha hizo ambazo zinakusanywa zinatumikaje katika kuwaletea maendeleo wananchi.
“Tangu tulipoanza ziara hii na leo ni siku ya tatu tumeona fedha za mapato ya ndani namna zilivyotumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, tunapeleka Pongezi kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko sababu ndiye aliunda kamati hii, pongeza pia kwa Mkurugenzi na Meya kwa usimamizi mzuri wa fedha hizo na leo tumeona mapinduzi makubwa ya maendeleo,”amesema Dk. Meshack.
Aidha, amesema utekelezaji huo wa miradi mbalimbali ya maendeleo utahamasisha wafanyabiashara kuendelea kulipa Kodi sababu wanaona fedha zao namna zinavyo rudi kwao kwa kutekelezewa miradi mbalimbali ya maendeleo, na uboreshaji wa miundombinu na kufanya biashara zao katika mazingira rafiki.
Pia amewasihi wafanyabiashara kuendelea kulipa kodi kwa hiari yao, ili Serikali ipate mapato mengi na kuwatekelezea miradi mbalimbali ya maendeleo kama inavyofanya hizi sasa ambapo mji wa Shinyanga umeshabadilika ndani ya muda mfupi kutokana na fedha za mapato ya ndani.
Naye Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, ambaye pi ndiye Mwenyekiti wa Kamati hiyo, amesema kuwa mji wa Shinyanga utajengwa na wananchi wenyewe na kuwasihi kuendelea kulipa mapato ili Serikali ipate fedha na kuwatekelezea miradi mbalimbali ya maendeleo na uboreshaji wa miundombinu zikiwamo barabara, Stendi, na ujenzi wa masoko.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati wa ya ukusanyaji mapato ya ndani halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga akizungumza kwenye ziara hiyo.
Katibu wa Kamati ya ukusanyaji mapato ya ndani halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Dk. Kulwa Meshack akizungumza kwenye ziara hiyo.
Wajumbe wa Kamati ya ukusanyaji mapato ya ndani halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye mradi wa machinjio ya kisasa Ndembezi ambao pia una mchango wa fedha za mapato ya ndani.
Ziara ikiendelea kwenye machanjio ya kisasa Ndembezi.
Ziara ikiendelea kwenye machanjio ya kisasa Ndembezi.
Ziara ikiendelea kwenye machanjio ya kisasa Ndembezi.
Ziara ikiendelea kwenye machanjio ya kisasa Ndembezi.
Muonekano wa machinjio ya kisasa.
Wajumbe wakiwa kwenye mradi wa ujenzi wa Stendi ya magari madogo (HIACE) eneo la Kambarage Manispaa ya Shinyanga ,ujenzi ambao utatumia mapato ya ndani Sh..milioni 211.
Muoenako wa Ramani ya ujenzi wa Stendi hiyo itakavyokuwa.
Wajumbe wakiwa kwenye ujenzi wa Soko la Machinga jirani na Ofisi ya CCM wilaya ya Shinyanga, ambapo wafanyabiashara watafanya biashara zao hadi majira ya usiku na linajengwa kupitia mapato ya ndani Sh.milioni 120.
Muonekano wa Stendi ya Magari madogo katika Soko kuu la Manispaa ya Shinyanga ambayo imeboreshwa kupitia mapato ya ndani Sh. milioni 147.
Wajumbe wakiwa katika ujenzi wa Zahanati ya Mwamagunguli Kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga ambayo imeshatengewa fedha Sh.milioni 60 kupitia fedha za mapato ya ndani ili kuendeleza ujenzi wake.
Wajumbe wakiwa katika Zahanati ya Bugweto Kata ya Ibadakuli ambayo nayo imeshatengewa Sh.milioni 30 kupitia fedha za mapato ya ndani ilikuendelea ujenzi wake huku fedha za Serikali ikitengewa Sh.milioni 50.
Social Plugin