Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AMUUA MKEWE KISHA KUJIUA CHANZO MICHEPUKO KISHAPU




picha hii haihusiani na tukio hilo

Na Halima Khoya Shinyanga

Mwanamke Mmoja mwenye umri wa Miaka 34, mkazi wa Mwamala kijiji cha Igumangobo Kata ya Idukilo Tarafa ya Mondo Wilaya ya Kishapu Mkoa Shinyanga, Getruda Paul ameuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo kifuani na shingoni na mumewe George Mahona (38) chanzo kikitajwa wivu wa kimapenzi akimtuhumu mkewe kuchepuka na mwanaume mwingine.


Tukio hilo limetokea Oktoba 19, 2022 mwaka huu majira ya saa moja asubuhi katika kijiji cha Igumangobo Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga.


Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Shinyanga, ACP Leornard Nyandahu amesema Getruda Paul ameuawa na mume wake, George Mahona kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kisha mwanaume huyo kujiua kwa kujinyonga chumbani kwao.


”Majira ya saa 1 asubuhi, jana tulipata taarifa ya tukio la mauaji ya Getruda Paul, ,aliyeuawa na George Mahona, ambaye ni Mumewe kwa kumtuhumu mkewe kuchepuka na mwanaume mwingine ambapo bado hajajulikana, mara baada ya kufanya mauaji hayo, Mtuhumiwa huyo alichukua jukumu la kujiua kwa kujinyonga na kamba ya chandarua”,amesema Nyandahu.


Amesema Miili yote ya marehemu hao ilifanyiwa uchunguzi katika Hospitali ya Serikali Wilaya Kishapu na imekabidhiwa kwa ndugu zao kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Nyandahu ametoa wito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi na kueleza kuwa upelelezi unaendelea ili kubaini undani wa tukio hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com