Jamal Shomari Mtepa anayekadiriwa kuwa na umri kati miaka 25 hadi 30 mkazi wa Kijiji cha Mchakama, Wilaya ya Kilwa, Mkoani Lindi ameuawa kwa kuchinjwa kwa kile kinachoelezwa kuwa alikunywa supu iliyokuwa imewekwa na rafiki yake aliyetajwa kwa jina la Akadwii.
Inaelezwa kuwa wawili hao walikuwa marafiki na siku ya tukio hilo Oktoba 24/2022 walienda pamoja kunywa pombe na waliacha supu nyumbani ambapo Mtepa aliwahi kurudi nyumbani na kuamua kuinywa supu hiyo
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mchakama, Mohamedi Waziri Mpinga amesema marehemu Mtepa na Akadwii ni marafiki na walikuwa na tabia ya kutembeleana na muda mwingine kila mmoja alikuwa analala kwa mwenzake.
“Huyu jamaa amemkata kichwa chote na kuacha sehemu kidogo ya ngozi kutenganisha kati ya kichwa na kiwiliwili”, alisema Mpinga.
Mpinga alisema siku hiyo ya Oktoba 24/2022,marafiki hao walikwenda kunywa Pombe, huku nyumbani kwao waliacha supu,hivyo Mtepa aliamua kurudi nyumbani kulala, huku akimuacha mwenzake akiendelea kunywa Pombe.
Alisema baada ya kufika Nyumbani Mtepa alichukua supu ya Ng’ombe na kuinywa kisha kulala usingizi, ambapo Akadwii aliporejea na kuangalia supu bila ya kuikuta, inaelezwa alichukuaa gongo na kumpiga Mtepa kichwani, hali iliyomstua usingizini na kuanza kugalala.
Mwenyekiti huyo wa Kijiji cha Mchakama amesema baada ya kuona hivyo, Akadwii alichukua kisu na kumchinja kwenye shingo kama kuku, huku akiwa amebakisha kiasi kidogo cha ngozi kutenganisha kichwa na kiwiliwili.
Alisema mtuhumiwa baada ya kutekeleza unyama huo, alivua nguo za marehemu na kuzivaa yeye kisha kuuchukua mwili na kwenda kuutelekeza kwenye mto Mavuji, huku miguu ikiwa ndani ya maji na kichwa nchi kavu.
Soma zaidi >>HAPA<<
Via EATV
Social Plugin