BODI YA NYAMA TANZANIA YASHAURI JAMII KUTUMIA NYAMA KUONDOKANA NA UTAPIAMLO


Msajili wa Bodi ya Nyama Tanzania Dkt. Daniel Mushi akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dodoma kwenye ukumbi wa Idara ya  Habari-Maelezo 


 Na Mwandishi wetu Dodoma.


Imeelezwa kuwa kitaalam na kiafya mtu mmoja anapaswa kula nyama wastani wa kilo moja kwa wiki  ikiwa ni njia moja wapo ya kuondokana na utapiamlo.


Hayo yameelezwa leo Oktoba 28 Jijini Dodoma na Msajili wa Bodi ya Nyama Tanzania Dkt. Daniel Mushi wakati Akielezea utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Bodi hiyo na mwelekeo wa utekelezaji kwa Mwaka wa Fedha wa 2022-2023,  na kuongeza kuwa ulaji wa nyama kwa Tanzani uko chini kwani mtu mmoja anakula kilo 25 kwa mwaka.


"Moja kati ya mikakati tuliyonayo ni kuhamasisha Watanzania kula nyama kwani kwasasa ulaji nyama uko chini kwani tunapaswa kula kilo walau 50 kwa mwaka,kwani kwa sasa mtu mmoja anakula kilo 25. Ulaji wa nyama kwa kiwango kinachotakiwa kunaweza kuwa njia ya kuondokana na utapiamlo"


Aidha Dkt.Mushi ameongeza kuwa ili mwili wa binadamu upate virutubisho vyote muhimu anatakiwa kwa wiki walau ale kilo moja ya nyama kwani virutubisho vinavyopatikana kwenye nyama nyekundu havipatikani kwenye mimea na kitaalamu mtu anapaswa kula nyama angalau kilo hamsini kwa mwaka.


Pia amesema kuwa endapo mtu atakula nyama kwa kiwango kinachotakiwa mtu huyo atakua na afya kwani itasaidia kuimarisha kinga ya mwili ya kupambana na magonjwa nyemelezi na kuongeza nguvu ya kufanya kazi hivyo itasaidia kuongeza uzalishaji.


"Kama mnavyo fahamu nyama ndio njia rahisi ya kuondokana na utapia mlo, mtu anapowaambia watanzania wasile nyama nadhani haelewi vizuri hali ilivyo katika ulaji wa nyama na sisi kama Serikali tunao mpango wa kuhamasisha watanzania wale nyama lakini ulaji nyama uliosahihi"


Katika hatua nyingine amesema kuwa bodi itahakikisha inalinda afya ya mlaji kupitia udhibiti na ukaguzi sambamba na kuhamasisha uzajishaji bora wa nyama ili kupata masoko nje ya nchi.


Kwasasa Mtanzania mmoja anakula nyama takribani kilo 25 kwa mwaka kuanzia Januari mpaka Disemba lakini tunapaswa kula nyama angalau kilo 50 kwa mwaka, kwa wenzetu Ulaya wanakula mpaka kilo 100 mtu mmoja kwa mwaka


"Sasa unapokula nyama kiasi kinachotakiwa kwanza unakuwa na afya unakuwa na nguvu ya kufanya kazi na uzalishaji unaongezeka lakini pia unakuwa na uwezo wa kinga ya mwili kuweza kujikinga na magonjwa kinga zinakuwa imara"


Mwaka 23006 serikali ilitunga sheria ya tasnia ya nyama sura ya 421 yenye lengo la kuwezesha mabadiliko katika tasnia ya nyama, kuanzisha misingi thabiti ya usimamizi, kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa bora za nyama, kuendeleza ukuaji wa tasnia ya nyama na bodi ya nyama Tanzania ilianzishwa katika sheria hii ili kusimamia utekelezaji wa sheria husika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post