Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KANISA LA IEAGT LA MTUNUKU CHETI CHA PONGEZI MKURUGENZI WA MANISPAA YA SHINYANGA KUUBADILISHA MJI KIMAENDELEO

Mchungaji wa Kanisa la IEAGT David Mabushi (kushoto) akimkabidhi cheti cha Pongezi Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura.

Mchungaji wa Kanisa la IEAGT David Mabushi (kushoto) akimkabidhi cheti cha Pongezi Afisa Utumishi wa Manispaa ya Shinyanga Getruda Gisema.

 

Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kukabidhi vyeti vya pongezi.

 Na Marco Maduhu, SHINYANGA

KANISA la International Evangelical Assemblies Of God (IEAGT) Mjini Shinyanga, limemtunuku cheti cha Pongezi Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, pamoja na watumishi kutokana na kazi kubwa ambayo wameifanya ya kuubadilisha mji huo kimaendeleo.


pongezi hizo za vyeti zimetolewa  leo Oktoba 21, 2022 katika Ofisi za Manispaa ya Shinyanga.
 
Mchungaji wa Kanisa hilo la IEAGT David Mabushi, amesema kwa kazi kubwa ambayo ameifanya Mkurugenzi huyo ya kuubadilisha mji wa Shinyanga kimaendeleo ndani ya muda mfupi, wameona siyo vyema kukaa kimya, bali wampatie pongezi ili kuendelea kumtia moyo na kuchapa kazi kwa bidii.

“Tangu Mkurugenzi umefika hapa Shinyanga tumeona umeubadilisha mji wetu kimaendeleo, hivyo tumeona sisi kama Kanisa tufike hapa Ofisini kwako ili tukupatie cheti chako cha Pongezi, na Cheti kingine kwa ajili ya watumishi sababu mmefanya kazi kubwa,”amesema Mabushi.

“Nawaombeni watumishi muendelee na moyo huo huo wa kufanya kazi kwa ushirikiano na Mkurugenzi wenu ili kuletea maendeleo wananchi, tumefurahi sana kuona mji wetu unabadilika, na sisi viongozi wa dini tutaendelea kuwaombea,”ameongeza.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, amesema cheti hicho cha pongezi ni deni kubwa kwake, katika kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo, huku akihidi kuendelea kuchapa kazi kwa bidii kwa kushirikiana na watumishi, na kuubadilisha mji huo kuwa na hadhi ya Makao Makuu ya Mkoa na kitovu cha kibiashara.

Amesema alipohamishiwa hapa Shinyanga Agost Mwaka jana na Rais Samia Suluh Hassan akitokea Lindi, walikaa na watumishi na kuainisha vipaumbele vyao vya kuubadilisha mji huo, na kuanza na uboreshaji wa utoaji wa huduma za kijamii ili kubadilisha ustawi wa maisha ya wananchi.

Amesema kitu kingine ni kuboresha miundombinu na kuweka mazingira mazuri ya wananchi kufanya biashara, sababu huo ndiyo wajibu wa Serikali katika kuandaa mazingira shawishi ya kibiashara.

“Nawashukuru viongozi wa dini kwa cheti hiki cha Pongezi pamoja na Cheti kingine kwa ajili ya watumishi, ni wahakikishie tu halmashauri ipo kwenye mikono salama, na huu ni mwanzo tu bali tuna mipango mingi ya kuubadilisha mji huu kimaendeleo,”amesema Satura.

Aidha, amewaomba watumishi wa halmashauri hiyo waendelee kuchapa kazi kwa bidii pamoja na ushirikiano, sababu hizo ndiyo nguzo kuu ya kusonga mbele kimaendeleo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com