WIKI mbili zilizopita kulikuwa na habari za tanzia kuhusu mwanamke mmoja aliyefariki dunia katika ajali ya barabara alipokuwa akimkimbiza mumewe, Sonnie Bassey baada ya kumfumania na mwanamke mwingine.
Sakata hilo limeibuka tena baada ya taarifa mpya kudai kuwa mwanaume yule naye pia amefariki dunia baada ya kuwa katika hali ya kutojitambua kwa majuma mawili tangu tukio lile kutokea, yeye akiwa kama mhusika mkuu katika kifo cha mkewe.
Kulingana na 9News, hatimaye mwanaume huyo kwa jina Sonnie alishindwa vita dhidi ya mshtuko uliompata na kufariki huku sasa watoto wao wakiwa wameachwa kama Yatima.
Gari lililopata ajali na kusababisha kifo cha mwanamke huyo
“Mke aliyefariki wiki mbili zilizopita alipomwona mumewe akitoka kwenye Shopping Mall ya SPAR akiwa na mwanamke mwingine alipojaribu kuzuia gari la mumewe na Toyota Highlander aliyokuwa akiendesha,” 9News iliripoti.
“Katika harakati za kumkimbia mumewe, alishindwa kulidhibiti gari lililokuwa likienda kwa kasi, na kuacha njia na kuligongesha gari lake kwenye mti, na kuharibu gari hilo kiasi cha kutorekebishwa na pia kujiua papo hapo,” habari zaidi zilisimulia.
Iliripotiwa kuwa baada ya kifo cha mkewe, mwanaume huyo alionekana akilia katika kitanda cha hospitali ambapo mwili wa mke wake ulikuwa umelazwa huku akibembeleza maiti hiyo kurudi ili waendelee kulea watoto wao, na pia akijutia tukio zima lililotokea.
Social Plugin