******************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KLABU ya Simba imeendelea kutoa dozi kwenye Ligi Kuu Tanzania NBC baada ya leo kuichapa Dodoma Jiji Fc kwa mabao 3-0, mchezo ambao ulipigwa katika dimba la Benjamini Mkapa.
Simba Sc imecheza mchezo huo siku chache baada ya kutoka visiwani Zanzibar kwaajili ya kujiweka sawa kwa michezo ya ligi kuu bara pamoja na ligi ya mabingwa Afrika ambayo michuano hiyo inaendelea wiki ijayo.
Simba imepata mabao yake kupitia kwa mshambuliaji wake Moses Phiri, Habibu Kyombo pamoja na bao lingine Dodoma Jiji wakijifunga wakijaribu kuokoa.
Social Plugin