Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NIC YAZINDUA MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA

Msajili wa Hazina Bw.Mgonya Benedicto akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Dkt. Elirehema Doriye akizindua Mkataba wa Huduma kwa Mteja wakati wa Maadhimisho ya Kimataifa ya Wiki ya Huduma kwa wateja iliyofanyika leo Oktoba 3,2022 Jijini Dar es Salaam. Msajili wa Hazina Bw.Mgonya Benedicto akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Dkt. Elirehema Doriye akizindua Mkataba wa Huduma kwa Mteja wakati wa Maadhimisho ya Kimataifa ya Wiki ya Huduma kwa wateja iliyofanyika leo Oktoba 3,2022 Jijini Dar es Salaam. Msajili wa Hazina Bw.Mgonya Benedicto akizungumza katika uzinduzi wa Mkataba wa Huduma kwa Mteja wakati wa Maadhimisho ya Kimataifa ya Wiki ya Huduma kwa wateja iliyofanyika leo Oktoba 3,2022 Jijini Dar es Salaam. Msajili wa Hazina Bw.Mgonya Benedicto akizungumza katika uzinduzi wa Mkataba wa Huduma kwa Mteja wakati wa Maadhimisho ya Kimataifa ya Wiki ya Huduma kwa wateja iliyofanyika leo Oktoba 3,2022 Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Dkt. Elirehema Doriye akizungumza katika uzinduzi wa Mkataba wa Huduma kwa Mteja wakati wa Maadhimisho ya Kimataifa ya Wiki ya Huduma kwa wateja iliyofanyika leo Oktoba 3,2022 Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wadau wa NIC wakifuatilia uzinduzi wa Mkataba wa Huduma kwa Mteja wakati wa Maadhimisho ya Kimataifa ya Wiki ya Huduma kwa wateja iliyofanyika leo Oktoba 3,2022 Jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Bima la Taifa (NIC) imezindua Mkataba wa Huduma kwa Mteja wakati wa Maadhimisho ya Kimataifa ya Wiki ya Huduma kwa wateja iliyofanyika leo Oktoba 3,2022 Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati akifungua huduma hiyo, Msajili wa Hazina Bw.Mgonya Benedicto amewataka watumishi wa NIC kufuata ahadi iliyowekwa kwenye mkataba huo na asiwepo mtumishi yeyote wa kutenda kinyume na mkataba huo kwani atachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria na Miongozo ya Utumishi wa Umma.

Amesema madhumuni ya mkataba huu ni kuboresha uhusiano baina ya Shirika na wateja wake lakini pia ukikusudia kuongeza uelewa kuhusu aina na ubora wa huduma zinazotolewa, haki na wajibu wa mteja na jinsi anavyoweza kuwasiliana.

"Mkataba wa Huduma kwa Mteja ni makubaliano kati yenu watoa huduma na mteja wenu ikiwa ni ahadi ya kutoa huduma bora kwa mteja, mkataba huu unaelekeza na kuainisha viwango vya huduma ambavyo wateja wenu wanatarajia kupata ili kufikia malengo yao". Amesema

Aidha amesema Ofisi ya Msajili wa Hazina na Serikali kwa ujumla ipo tayari kuwapa ushirikiano mnaostahili ikiwa tu mtaweka bidii katika kazi na kuboresha huduma zaidi ya zilivyo sasa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Dkt. Elirehema Doriye, amesema Shirika limekuwa likifanya mabadilikko kwenye kuwahudumia wateja ambapo wamekuwa wakiboresha huduma ili kuendana na ushindani ulioko sokoni jambo lililowavutia wateja kununua bidhaa zao za Bima na kuwafanya kuwa na ukuaji wa faida ya zaidi ya asilimia 100 katika miaka minne mfululizo.

"Mojawapo ya misingi inayotuongoza NIC yetu ni kutambua kuwa siku zote "Mteja Kwanza" yaani "Customer first" hii inamaanisha kwamba mteja kwetu ni kipaumbele namba moja katika utoaji huduma". Amesema Dkt.Doriye.

Aidha Dkt.Doriye amesema katika kuadhimisha wiki hii na kutambua umuhimu wa wateja, Shirika limezindua Mkataba wa Huduma kwa Mteja "ikiwa ni ahadi yetu kwa wateja kuwa tutawapatia huduma inayostahili kulingana na ahadi tuliyowapa". Amesema

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com