BALOZI WA UINGEREZA NCHINI TANZANIA AWAPA POLISI MBINU KUKABILIANA NA MAJANGA




Na. Abel Paul Jeshi la Polisi- Dar es salaam
22.10.2022

Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, David Concar amesema kuwa maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi wanapaswa kuwa makini na uwasilishwaji wa taarifa kwa umma ili kuepuka baadhi ya watu wengine kuzibadilisha taarifa kwa lengo la kupotosha wananchi wakati wa majanga na dharura.


 Balozi David Concar amesama hayo mapema leo October 22.2022 wakati akufunga mafunzo awamu ya pili ya kuwajengea uwezo wa mawasiliano maafisa wa Jeshi hilo  wakati wa majanga na dharura yaliyofanyika jijini Dar es salaam ambapo mafunzo hayo yalianza tarehe 18 hadi 22 october mwaka huu.

Kwa upande wake Kamishina wa intelijensia ya makosa ya Jinai CP CHARLES MKUMBO amewataka washiriki kutumia mafuzo hayo vizuri ambapo yatawajengea uwezo mkubwa wa kutoa taarifa zinazozingatia vigezo ili kuepuka kutoa taarifa za upotosha katika jamii.

CP Mkumbo Pia amewashukuru wafadhiri wa mafunzo hayo kutoka ubalozi wa Uingereza, taasisi ya Mercy Corps pamoja na wawezeshaji kutoka chuo kikuu Dar es salaam kwa kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo kwa kupambana na majanga ya dharura pindi yanapotokea.
  
Aidha Bi. JESSIE BEHAM mmoja wa wawezeshaji wa mafunzo hayo kutoka taasisi ya global communications academy ya nchini uingereza, amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa maofisa wa Polisi na maofisa wa serikali kwa ujumla ambapo amebainisha kuwa yatawajengea uwezo uwezo  katika kufanya mawasiliano wakati wa dharura na majanga pindi yanapotokea.

Pia Bw. ANTHONY SAROTA ambae pia nimratibu wa shirika la mercy corps Tanzania amesema kuwa baada ya matokeo mazuri ya mafunzo hayo, amebainisha kuwa malengo ya shirika hilo ni kuwezesha askari wa Jeshi la Polisi Nchini kuweza kufundishana nakuwafikia maofisa n askari wa Jeshi hilo  Nchi nzima.

Nae DR. RICHARD SAMBAIGA mmoja wa wawezeshaji wa mafunzo hayo kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam, amesema mafunzo hayo yatawajengea uwezo kwa kutambua msingi na sayansi katika mawasiliano na namna ya kufanya kukabiliana na majanga nchini

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post