HUDUMA YA MATIBABU YA MACHO BURE YAMKOSHA RC MJEMA...AMPONGEZA MBUNGE LUCY MAYENGA KUONGEZA FURAHA KWA WANANCHI



Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akipima Macho akiwa na Mbunge wa Vitimaalum wa Mkoa huo Lucy Mayenga, alipofanya ziara ya kukagua zoezi la utolewaji matibabu ya macho bure kwa wananchi wa Shinyanga kutoka kwa Madaktari Bingwa wa Macho zoezi lililoratibiwa na Mbunge Lucy Mayenga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akipima Macho alipofanya ziara ya kukagua zoezi la utolewaji matibabu ya macho bure kwa wananchi wa Shinyanga ,kutoka kwa Madaktari Bingwa wa Macho zoezi lililoratibiwa na Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, ametembelea kuona zoezi la wananchi wa Mkoa huo wakipatiwa huduma ya matibabu ya macho bure, ambalo limeratibiwa na Mbunge wa Vitimaalum mkoani humo Lucy Mayenga.  

Mjema amefanya ziara hiyo leo Oktoba 16, 2022, ambapo zoezi hilo la utoaji matibabu bure ya macho lilianza rasmi Oktoba 14 mwaka huu na linahitimishwa leo, na lilikuwa likifanyika katika chuo cha Ualimu Shinyanga (SHYCOM) pamoja na Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya wagonjwa waliohitajika kufanyiwa upasuaji.


Akizungumza katika ziara hiyo amempongeza Mbunge Lucy Mayenga, kwa kuguswa na kuratibu matibabu hayo, ambayo wananchi wamepatiwa tiba bure ya macho, na ambao walikuwa hawaoni kabisa sasa wanaona na watakwenda kufanya shughuli za maendeleo.


“Mbunge Lucy Mayenga ni Mbunge Machachari sana, anafanya kazi na ana Roho ya kupenda wananchi wake, ndiyo maana ameratibu matibabu haya ya macho ili wananchi watibiwe na huduma hii imetolewa bure kabisa,” amesema Mjema.


“Tumpongeze pia Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa kuifungua Tanzania, sababu bila yeye madaktari hawa bingwa wa macho wasinge weza kuja kutoa huduma hii ya matibabu ya macho kwa wananchi wetu hapa Shinyanga,”ameongeza.


Aidha, amewaomba Madaktari hao bingwa wa macho wasichoke kuja mkoani Shinyanga kuendelea kutoa tiba hiyo ya macho, sababu bado kuna uhitaji mkubwa wa wananchi kapata huduma hiyo, na ikiwezekana waje tena Januari mwakani.

Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoani Shinyanga Dk, John Luzila, amepongeza huduma hiyo ya matibabu ya macho kwa wananchi wa Mkoa huo, na kubainisha kuwa pia Serikali imeshapeleka daktari wake masomoni, ambaye anasomea ubingwa wa matatizo ya macho na atakuwa akifanya kazi katika hospitali hiyo.

Aidha, Mbunge Lucy Mayenga, amesema baada ya kuona katika Mkoa huo kuna upungufu wa madaktari bingwa wa macho, ndipo akaona ni vyema aratibu matibabu hayo ili wananchi wapate huduma bure, sababu baadhi yao hawezi kumudu gharama za matibabu kwenda katika hospitali kubwa.

Amesema pia katika nafasi yake ya ubunge atalipigia kelele suala hilo la upatikanaji wa madaktari bingwa wa macho katika Hospitali mbalimbali hapa nchini ukiwemo na Mkoa wa Shinyanga, ili wananchi wapate matibabu kwa urahisi.

Nao baadhi ya wananchi waliopewa huduma hiyo akiwemo Happines Williamu, amesema tangu mwaka 2013 aligunduliwa kuwa na tatizo la mtoto wa jicho, lakini kutokana na ukosefu wa fedha za matibabu ilibidi akae bila tiba hadi jana ndipo akafanyiwa upasuaji bure, na sasa macho yake yote ni mazima na anaona vizuri.

Kwa upande wake Mratibu wa Taasisi ya Bilal Muslim Mission Of Tanzania Free eye Camp, ambaye pia ni kiongozi wa jopo la madaktari hao bingwa wa macho Ain Sharif, kwa kushirikiana na Beta Charitable Trust ya Uingereza, amesema katika Mkoa huo wa Shinyanga wamevunja Rekodi ya utoaji wa matibabu bure ya macho, kuwa ndani ya miaka yao 25 hawajawahi kuwafanyiwa watu 116 upasuaji wa macho kwa siku moja, na kwa siku hizo tatu jumla ya wananchi 167 wamefanyiwa upasuaji na bado zoezi linaendelea kwa siku ya leo.

Amesema kutokana na bado kuna uhitaji wa watu wengi bado hawajapata matibabu hayo ya macho na muda umeshakwisha, itabidi baadhi ya madaktari wao wabaki kuendelea na huduma hiyo kwa siku kadhaa.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akizungumza kwenye zoezi la utoaji matibabu ya macho bure, lililoratibiwa na Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga.

Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga akielezea namna alivyoguswa na kuratibu matibabu hayo ya Macho na kuleta madaktari bingwa wa macho mkoani Shinyanga na kutoa huduma bure kwa wananchi.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dk. John Luzila akizungumza kwenye uhitimishaji wa zoezi hilo la utoaji matibabu ya macho bure mkoani Shinyanga kutoka kwa madaktari bingwa wa macho.

Mratibu wa Taasisi ya Bilal Muslim Missioni Of Tanzania Free Eye Camp Ain Sharif akielezea namna walivyotoa matibabu hayo ya macho kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga.

Mwananchi Happines Wiliam akielezea namna alivyopata huduma ya matibabu ya macho na sasa anaona vizuri tofauti na hapo awali.

Mwanachi George Mwandu akielezea namna alivyopata matibabu ya macho.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akiangalia namna wananchi wanavyopata huduma ya matibabu ya macho bure kutoka kwa madaktari bingwa wa macho.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akipokea maelezo kutoka kwa Madaktari bingwa wa macho namna wanavyotoa huduma.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akipokea maelezo kutoka kwa Madaktari bingwa wa macho namna wanavyotoa huduma.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema (kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa Mratibu wa Taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania Free Eye Camp Ain Sharif namna wanavyotoa huduma ya matibabu ya macho.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema (kulia) akipokea maelezo kutoka kwa Mratibu wa Taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania Free Eye Camp Ain Sharif namna wanavyotoa huduma ya matibabu ya macho, katikati ni Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akipima Macho akiwa na Mbunge wa Vitimaalum wa Mkoa huo Lucy Mayenga, alipofanya ziara ya kukagua zoezi la utolewaji matibabu ya macho bure kwa wananchi wa Shinyanga kutoka kwa Madaktari Bingwa wa Macho zoezi lililoratibiwa na Mbunge Lucy Mayenga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akipima Macho akiwa na Mbunge wa Vitimaalum wa Mkoa huo Lucy Mayenga, alipofanya ziara ya kukagua zoezi la utolewaji matibabu ya macho bure kwa wananchi wa Shinyanga kutoka kwa Madaktari Bingwa wa Macho zoezi lililoratibiwa na Mbunge Lucy Mayenga.

Afisa wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Jackson Mwakagonda akipima macho.

Zoezi la upimaji macho likiendelea.

Zoezi la upimaji macho likiendelea.

Zoezi la upimaji macho likiendelea.

Zoezi la upimaji macho likiendelea.

Zoezi la upimaji macho likiendelea.

Zoezi la upimaji macho likiendelea.

Zoezi la upimaji macho likiendelea.

Daktari Bingwa wa Macho Nazneen Shariff akimwekea dawa ya macho Mwananchi Chambi Ndinganya.

Matibabu ya macho yakiendelea na uwekaji wa dawa za macho.

Matibabu ya macho yakiendelea na uwekaji wa dawa za macho.
Daktari Bingwa wa Macho Dk, Secodri Njau akitoa elimu ya matumizi ya dawa na namna ya kulinda macho yao kwa wananchi ambao wamefanyiwa upasuaji wa macho.

Wananchi wakiendelea kusikiliza elimu ya matumizi ya dawa na namna ya kulinda macho yao.

Wananchi wakiendelea kusikiliza elimu ya matumizi ya dawa na namna ya kulinda macho yao.

Wananchi wakiendelea kusikiliza elimu ya matumizi ya dawa na namna ya kulinda macho yao.

Baadhi ya Madaktari bingwa wa macho kutoka Taasisi ya Bilali Muslim Mission of Tanzania Free Eye Camp akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akizungumza na wananchi waliopata matibabu ya macho.

Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga, (kushoto) akimkabidhi msaada wa magongo ya kutembelea Bibi Marry Dotto, ambaye pia alifika kupata huduma ya matibabu ya macho kutoka kwa madaktari bingwa wa macho.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, akiwa katika ziara ya kujionea namna wananchi wa Mkoa huo wanavyopata huduma ya matibabu ya macho bure kutoka kwa madaktari bingwa wa macho kutoka Taasisi ya Bilal Muslim Mission Of Tanzania Free Eye Camp, zoezi ambalo limehitishwa leo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post