*****************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KLABU ya Simba imeamua kuifanyia ukatili Mtibwa Sugar baada ya kuinyeshea mvua ya magoli 5-0 na kuondoka na ushindi huo muhimu wa ligi kuu Tanzania bara.
Kipindi cha kwanza Simba Sc ilifanikiwa kupata bao kupitia kwa Mzamiru na kuwapeleka mapumziko wakiwa mbele ya bao 1-0 huku Mtibwa akiwa nusu baada ya mchezaji wake Kitenge kupewa kandi nyekundu.
Kipindi cha pili Simba iliendelea kutoa dozi ya nguvu kwenye mchezo glhuo baada ya kuongeza mabao mengine na kufikia 5-0 huku Mtibwa tena akipewa kadi nyekundu mchezaji wake Cassian baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano.
Mabao ya Simba Sc mengine yamefungwa na Okra, Moses Phiri,Sakho ambaye amepachika mabao mawili kwenye mchezo huo
Social Plugin