*****************
NA MWANDISHI WETU
SHIRIKA la Viwango Tanzania limeshiriki katika Maonesho ya Tano ya Sekta ya Madini yanayofanyika Mkoani Geita ambapo wameendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa uzalishaji na uuzaji wa bidhaa zenye ubora na viwango.
Akizungumza na Mwandishi wetu kwenye Maonesho hayo leo Oktoba 7,2022 Meneja wa TBS Kanda ya Ziwa, Mhandisi Joseph Mwaipaja amesema ili kuweza kuuza vitu ama chakula kwenye migodi lazima vitu hivyo ama chakula kiwe bora na kuthibitishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Amesema ni fursa kwa wananchi wa mkoani Geita na mikoa jirani kuweza kutembelea banda la TBS na kuweza kupewa elimu ya udhibiti ubora ili kuzalisha na kununua biidhaa zilizokidhi viwango .
"Ni fursa kwa wakulima kuzalisha bidhaa na kuthibitishwa na TBS, kwaajili ya biashara ndani na nje ya nchi, kwani nchi za jirani zimekuwa zikitegemea bidhaa zetu kama mchele hivyo tunatakiwa kuzalisha bidhaa zilizo na ubora". Amesema
Social Plugin