TEMDO YAJA NA SULUHISHO LA SUMU KUVU KATIKA ZAO LA MIHOGO






Afisa wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko Dkt. Sigisbert Mmasi kutoka Taasisi ya ubunifu na Usanifu mitambi Tanzania (TEMDO)akitoa maelezo Kwa naibu Katibu Mkuu wa wizara ya uwekezaji ,viwanja na biashara Ally Gugu pamoja baadhi ya wananchi waliotembelea banda lao lililopo katika maonyesho ya 17 ya SIDO Kanda ya kaskazini yanayofanyika katika viwanja vya makumbusho vilivyopo ndani ya halmashauri ya jiji la Arusha mkoani Arusha


Na Woinde Shizza,Arusha

Tatizo la kumaliza uwepo wa sumu kuvu katika zao la muhogo limepatiwa ufumbuzi na Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) mara baada ya kuwabunia wakulima wa zao hiyo mtambo utakao wasaidia kuchakata zao hilo mara tu baada ya kuvunwa .



Hayo yamebainishwa na Ofisa wa kitengo cha Mawasiliano na Masoko Dkt. Sigisbert Mmasi kutoka Taasisi ya ubunifu na Usanifu mitambi Tanzania (TEMDO) wakati akiongea katika maonyesho ya 17 ya SIDO Kanda ya kaskazini yanayofanyika katika viwanja vya makumbusho vilivyopo ndani ya halmashauri ya jiji la Arusha mkoani Arusha ambapo alisema kuwa mashine hiyo itamkomboa sana mkulima wa zao la muogo.



Alisema kuwa Mtambo huu utakuwa mkombozi kwa wakulima kwakuwa muhogo ukivunwa unatakiwa uchakatwe mapema maana ukikaa sana unaweza ukaharibika ,ukatengeneza sumu kuvu ambayo ni Kuvu/ukungu/fangasi hushambulia mazao mbalimbali ya chakula, ambapo kawaida kuvu hupatikana kwenye udongo wakati wote katika hali ya vumbi au muhogo huo ukaharibika ukawa haufai tena kwa matumizi ya binadamu.


Alibainisha kuwa Temdo kila mwaka wanakuja na kitu kipya ambacho kitamsaidia mkulima katika kazi zake pamoja na kutatua matatizo katika kilimo anachofanya ,na kwa mwaka huu wameamua kumletea mkulima mtambo huo ambao utamsaidia mkulima kuokoa mazao yake ambayo yalikuwa yakiaribika kutokana na kukosa soko



Alisema kuwa mtambo huo unauwezo wa kuchakata zao la muhogo takribani tani 12 na wenyewe unakuwa na tani elfu 12000 za muhogo ambapo ukichakata unapata unga takribani tani tatu.

“Mtambo huu ni wa kisasa na unamsaidia mkulima kwa sababu unauwezo wa kuvuna muhogo siku hiyo hiyo na kuchakata siku hiyo hiyo ,na niwaambie ukishavuna muhogo wako unaumenya unaingiza kwenye mashine unatengenezwa uji baada ya apo unawekwa kwenye draya ambayo inasaidia kukausha ule unga wa muhogo siku hiyo hiyo kwa iyo unapata unga siku hiyo hiyo ,na unaweza kupeleka kwa walaji siku hiyo hiyo", alibainisha Mmasi.

Alisema kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa ya kutokuwa na mvua kwa kipindi kirefu mtambo huo utasaidia kuokoa kile chakula ambacho kilikuwa kinapotea kwa kuoza bure kutokana na kukaa mda mrefu bila kuchakatwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post