Mkurugenzi wa Tiba wa Wizara ya Afya Profesa Paschal Lugajo .
Na Dotto Kwilasa,DODOMA.
IMEELEZWA kuwa takribani watu milioni 18 hufariki kila mwaka Duniani kote kutokana na maumivu na mateso kutokana na kukosa huduma ya udhibiti wa maumivu ambapo watu wazima ni asilimia 83 na asilimia 98 ni watoto.
Kutokana na hali hiyo ,Serikali kupitia wizara ya Afya nchini imesema itaanza kutoa kipaumbele kwenye tiba shafaa katika jamii Ili kuono wahanga wa tatizo hilo ambalo kati ya watu 218 mmoja kati yao anasumbuliwana na ugonjwa wa shufaa .
Kauli hiyo imetolewa jana Jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Tiba wa Wizara ya Afya Profesa Paschal Lugajo kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Serikali kuhusu kilele cha Siku ya Tiba Shufaa Duniani kote ambayo huadhimishwa kila ifikapo Oktoba 8 Mwaka huu.
Profesa Lugajo amesema kuwa hali hiyo imekuwa inachangiwa na uwepo wa vituo vichache vyenye watalaam wa huduma hizo za Tiba shufaa pamoja na uelewa mdogo wa jamii kuhusu huduma hizo.
Sanjari na hilo amesema kuwa kutokana na kuwepo kwa tatizo Hilo Wizara ya Afya ipo katika mchakato wa kuandaa Mitaala ya mafunzo ya Tiba shufaa kutokana na watu kupata msongo wa mawazo pale wanapoondokewa na ndugu zao hasa wenza na hupelekea kujidhuru.
Profesa Lugajo amebainisha kuwa kupitia juhudi zetu za pamoja, Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Watalaam wa Huduma za Afya, Viongozi wa Madhehebu ya Dini, Taasisi za Kijamii ili kuweza “Kuponya MPPioyo na Jamii’’.
Amesema Serikali inatambua kwamba kifo, kufa na huzuni havitenganishwi na kwamba Huduma za Tiba Shufaa inajumuisha kuwasaidia wale wote wenye huzuni itokanayo na kufiwa na mpendwa wao wa karibu baada ya kumuuguza kwa muda mrefu bila kujali umri wake.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa Kwa juma zima la kwanza la Mwezi huu Oktoba 2022 yaani kuanzia tarehe 01-08 Oktoba 2022 Timu za watalaam wa Huduma za Tiba Shufaa wamekuwa wakitoa huduma hizi katika Vituo mbalimbali vya huduma za Afya pamoja na kutoa elimu katika Vyombo vya Habari.
“Ninaamini kuwa Uhamasishaji uliofanywa katika juma hili umeweza kuongeza ufahamu kwa jamii iliyopata huduma hizi za Tiba Shufaa ambayo ni sehemu ya haki ya afya kwa wananchi, falsafa ambayo itaisaidia jamii kupunguza mateso yatokanayo na kuuguza”,amesema
Social Plugin