Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amemteua Innocent Bashungwa, aliyekuwa Waziri wa TAMISEMI kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Pia amemteua Dkt. Stergomena Lawrence Tax kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ambaye amechukua nafasi ya Balozi Liberata Mulamula.
Aidha amemteua Angellah Jasmine Kairuki, kuwa Mbunge na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Social Plugin