WAZIRI DKT.KIJAJI AZINDUA BODI YA WRRB, ASISITIZA UCHAPA KAZI

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt.Ashatu Kijaji akimkabidhi vitendeakazi mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) Bw.Arafat Haji mara baada ya kuzindua Bodi hiyo leo Oktoba 28,2022 Jijini Dar es Salaam.   Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt.Ashatu Kijaji akikabidhi vitendeakazi kwa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) mara baada ya kuzindua Bodi hiyo leo Oktoba 28,2022 Jijini Dar es Salaam Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt.Ashatu Kijaji akizungumza mara baada ya kuzindua Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) leo Oktoba 28,2022 Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) Prof. Geraldine Rasheli akizungumza katika uzinduzi wa Bodi hiyo iliyozinduliwa leo Oktoba 28,2022 Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) wakifuatilia uzinduzi wa Bodi hiyo leo Oktoba 28,2022 Jijini Dar es Salaam.Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt.Ashatu Kijaji akipata picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya WRRB Prof. Geraldine Rasheli na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB)Bw. Asangye Bangu wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika eo Oktoba 28,2022 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt.Ashatu Kijaji akipata picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo iliofanyika leo Oktoba 28,2022 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

***********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt.Ashatu Kijaji ameitaka Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) kuhimiza usindikaji wa mazao ya msingi nchini kwa lengo la kuongeza thamani na kukuza uendelezaji wa viwanda pamoja na kuongeza upatikanaji wa sehemu zilizo bora za kuhifadhia mazao.

Amesema hii itasaidia kupunguza hasara za baada ya kuvuna na kuimarisha uhakika wa chakula na kuongeza wigo wa wananchi kuweza kukopa katika asasi za fedha kwa kutumia mazao yao kama dhamana.

Ameyasema hayo leo Oktoba 28,2022 wakatti akizindua Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) Jijini Dar es Salaam ambapo ameitaka Menejimenti kuhakikisha wadau hususan Sekta Binafsi ikiwemo Waendesha Ghala na Benki wanaandaa utaratibu maalum wa mikopo ya ujenzi wa Ghala katika maeneo ya kimkakati ya Bodi ili kutoa mbadala wa njia ya mzalisha mali kufika sokoni.

Aidha Dkt.Kijaji ameitaka Bodi kusimamia kukuza juhudi za Serikali kurasimisha mifumo ya masoko iliyopo kwa lengo la kupunguza vipingamizi mbalimbali vinavyokwaza uzalishaji wenye tija na utafutaji masoko kwa bidhaa mbalimbali hususan mazao ya kilimo.

"Mfumo huu una manufaa mbalimbali ikiwemo kuwapa nguvu waweka mali hususan wakulima kupigania bei nzuri katika soko kwa kuhamasisha kutumia mfumo wa pamoja kukusanya na kuuza, kutoa uhakika wa ubora na bidhaa na mfumo wa uthibitisho". Amesema

Amesema Bodi inatakiwa kuhakikisha wanaishauri taasisi katika mambo mbalimbali ndani na nje ya vikao vya Bodi. Ushauri ni katika maeneo mengi yenye tija kwa taasisi, ikiwemo utatuzi wa changamoto zinazojitokeza.

"Bodi inatarajiwa iwe juu ya majanga yote yanayoweza kuikumba taasisi ili Bodi iendelee kuwa na maana machoni mwa watumishi, umma na Serikali". Amesema Dkt.Kijaji.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya WRRB Prof. Geraldine Rasheli amesema watajitahidi kuhakikisha kunakuwa na mijadala yenye afya kwa taasisi pamoja na kujituma huku wakizingatia masilahi mapana ya taasisi, Wizara, Serikali na Umma kwa ujumla wake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post